Mkuu nashukuru sana kwa info. nimeingia nimesoma taratibu zote ila bado naomba msaada zaidi.
Hii ni NGO ambayo imesajiliwa tayari huko ujerumani kinachotakiwa ni kuwa na ofisi au ukipenda unaweza kuiita tawi hapa Tanzania.
Swali: je ni lazima kuanza taratibu kama ndo kama vile inaanza? Au ni kupresent docs za usajili wa ujerumani kwa wizara husika?
Asante
Ndugu,
Zingatia hapo kwenye swali lako nililobold;
Ndio ni vyema kuanza kwa kufuata taratibu zilizoainishwa pale kwenye kiambatanisho cha awali kwani kwa Tanzania ndio itakuwa INAANZA operation, (Nakala za vyeti pamoja na Katiba ya hiyo Taasisi vyote vitapaswa kuambatanishwa). Sasa kwa kuwa ni tumeshakuwekea mawasiliano ya wadau wanaohusika na mchakato huo basi ni vyema ungewasiliana na mamlaka husika kwa Maelezo zaidi.
Lakini kama nilivyokueleza awali Taasisi hizi husajiliwa chini ya sheria tofauti tofauti kama vile Sheria ya Vyama, Sura 337, Sheria ya Udhamini, Sura 375 na Sheria ya Makampuni, Sura 212/213. Sasa kwa kuwa hatuna ufahamu wa muundo na malengo ya shirika lenu inatuwia vigumu sana kuwashauri ipasavyo, hata hivyo, tunaweza kuwapatia picha kidogo, (na hapa tutaassume kuwa awali Taasisi yenu ilisajiliwa kama NGO lakini yenye muundo wa Kampuni)
Usajili
Inakupaswa uelewe kuwa kuna mashirika Makubwa ya Kimataifa yaliyosajiliwa kama NGO huko kwao, lakini yana hadhi ya kampuni lisilokuwa na mtaji, yaani Company Limited by Guarantee, not having a share capital
Sasa ili Shirika kama hilo liweze kufanya Shughuli zake kihalali hapa Tanzania ni lazima kwanza likidhi matakwa ya Sheria ya Makampuni (The Companies Act Cap 212), yaan lisajiliwe kwa mujibu wa part XII of Cap.212 kwa kuwa awali lilisajiliwa nje ya Tanzania
(
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa shirika kama Foundation for International Community Assistance wengi wakilifahamu kama FINCA)
Foreign companies (companies incorporated out of Tanzania)
# These are companies incorporated outside Tanzania. Their offices in Tanzania are treated as branches of foreign company. They are registered under part XII of Cap.212
# The Registration procedure of this type of companies include the submission of :-
>Certified copies of Memorandum and Articles of Association.
>Notice of the location of the registered office in the country of domicile.
>List of Directors of the company.
>
Persons resident in the country who are the representatives of the company
Baada ya kupata hiyo certificate kutoka BRELA ndio unakwenda kwa Registrar of NGO kuomba Cheti cha Ukubalifu (Certificate of Compliance) kama ilivyoelekezwa kwenye kile kiambatanisho cha awali.
Ukitaka Ushauri wa Uhakika ni vyema ukawa muwazi, kwa kutupatia taarifa sahihi na zilizojitosheleza. Lakini kutokana na suala la kiusalama na usiri ni vyema ukawasiliana na Taasisi husika kwa Maelezo zaidi