Msaada; kufungua office yenye makao yake makuu nje

kajansi

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
485
Reaction score
222
Habari za pasaka wanajamvi!

Naomba kujuzwa utaratibu! Nimepata kibarua kama consultant kwenye NGO moja iliyopo Ujerumani na wanataka kufungua office hapa kanda ya ziwa ikiwa na staff mmoja toka huko lakini mshahara atakuwa anawekewa huko kwa ac ya kwao!
Je nini kinatakiwa ili kuweza kufungua hii office? au niende office zipi ambazo naweza pata msaada?

Asanteni.
 
Mkuu kama Ni NGO maana yake ni mpaka ifanye Regstration Tanzania, yaani ili kufanya kazi Bongo ni lazimaisajiliwe Tanzania, na hakuna njia nyingine, na nilisikia kwa Ishu ya NGO za nje usajili unafanyika wizara ya mambo ya dani ila kwa NGO za huku huku bongo ndo wamehamisha wizara, na NGO za nje uajili unafanyika hapo kwa sababu ya sensitivity yake
 
Asante sana mkuu chasha! Jingine vipi habari ya roosters umepata? au ujaingia pande za kenya?
 
Nafanyia kazi, so nitawaalifu make nafikilia bora kubeba mayai ambyo ni fertilized
 
Habari za pasaka wanajamvi!

Naomba kujuzwa utaratibu! Nimepata kibarua kama consultant kwenye NGO moja iliyopo Ujerumani na wanataka kufungua office hapa kanda ya ziwa ikiwa na staff mmoja toka huko lakini mshahara atakuwa anawekewa huko kwa ac ya kwao!
Je nini kinatakiwa ili kuweza kufungua hii office? au niende office zipi ambazo naweza pata msaada?

Asanteni.

Ndugu,
Kuna asasi tofauti zanazosajiliwa chini ya sheria tofauti hapa Tanzania (ingawa wengine wanaziita kama NGOs, lakini kiuhalisia zinakuwa hazijasajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali- NGO) Hivyo ingetuwia rahisi kukushauri vizuri kama tungetambua malengo na muundo wa hilo shirika lenu.

Kimsingi NGO zinasajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali yaan THE NON GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS ACT, NO. 24/2002. Na zinasimamiwa na Sera ya Taifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka
2001. THE NATIONAL POLICY ON NON-GOVERMENTAL ORGANIZATIONS

Awali ofisi ya Msajili ilikuwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Raisi lakini kwa sasa Ofisi hii inapatika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Anuani yao ni
Msajili wa NGOs
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
S.L.P 3448
Dar es Salaam
Simu 022 2113857/ 2123143
Tovuti. Tanzania Non-Government Organisation [NGO] - National Coordination
 
Kama shirika lenu hilo lilishasajiliwa kama NGO huko Ujerumani basi taratibu za kufuata hapa sio ngumu sana.
Kwa Taarifa zaidi tufuatilie kwenye twitter kupitia http://twitter.com/SongambeleEN. Kwa sasa kuna tumeattach document rasmi inayoelezea taratibu za Usajili wa NGO, inapatikana http://t.co/BXuT7yfxFU.
 
Mkuu nashukuru sana kwa info. nimeingia nimesoma taratibu zote ila bado naomba msaada zaidi.

Hii ni NGO ambayo imesajiliwa tayari huko ujerumani kinachotakiwa ni kuwa na ofisi au ukipenda unaweza kuiita tawi hapa Tanzania.
Swali: je ni lazima kuanza taratibu kama ndo kama vile inaanza? Au ni kupresent docs za usajili wa ujerumani kwa wizara husika?

Asante
 
Zingatia hapo kwenye swali lako nililobold; Ndio ni vyema kuanza kwa kufuata taratibu zilizoainishwa pale kwenye kiambatanisho cha awali kwani kwa Tanzania ndio itakuwa INAANZA operation, (Nakala za vyeti pamoja na Katiba ya hiyo Taasisi vyote vitapaswa kuambatanishwa). Sasa kwa kuwa ni tumeshakuwekea mawasiliano ya wadau wanaohusika na mchakato huo basi ni vyema ungewasiliana na mamlaka husika kwa Maelezo zaidi.

Lakini kama nilivyokueleza awali Taasisi hizi husajiliwa chini ya sheria tofauti tofauti kama vile Sheria ya Vyama, Sura 337, Sheria ya Udhamini, Sura 375 na Sheria ya Makampuni, Sura 212/213. Sasa kwa kuwa hatuna ufahamu wa muundo na malengo ya shirika lenu inatuwia vigumu sana kuwashauri ipasavyo, hata hivyo, tunaweza kuwapatia picha kidogo, (na hapa tutaassume kuwa awali Taasisi yenu ilisajiliwa kama NGO lakini yenye muundo wa Kampuni)

Usajili
Inakupaswa uelewe kuwa kuna mashirika Makubwa ya Kimataifa yaliyosajiliwa kama NGO huko kwao, lakini yana hadhi ya kampuni lisilokuwa na mtaji, yaani Company Limited by Guarantee, not having a share capital
Sasa ili Shirika kama hilo liweze kufanya Shughuli zake kihalali hapa Tanzania ni lazima kwanza likidhi matakwa ya Sheria ya Makampuni (The Companies Act Cap 212), yaan lisajiliwe kwa mujibu wa part XII of Cap.212 kwa kuwa awali lilisajiliwa nje ya Tanzania
(Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa shirika kama Foundation for International Community Assistance wengi wakilifahamu kama FINCA)

Foreign companies (companies incorporated out of Tanzania)
# These are companies incorporated outside Tanzania. Their offices in Tanzania are treated as branches of foreign company. They are registered under part XII of Cap.212
# The Registration procedure of this type of companies include the submission of :-
>Certified copies of Memorandum and Articles of Association.
>Notice of the location of the registered office in the country of domicile.
>List of Directors of the company.
>Persons resident in the country who are the representatives of the company

Baada ya kupata hiyo certificate kutoka BRELA ndio unakwenda kwa Registrar of NGO kuomba Cheti cha Ukubalifu (Certificate of Compliance) kama ilivyoelekezwa kwenye kile kiambatanisho cha awali.

Ukitaka Ushauri wa Uhakika ni vyema ukawa muwazi, kwa kutupatia taarifa sahihi na zilizojitosheleza. Lakini kutokana na suala la kiusalama na usiri ni vyema ukawasiliana na Taasisi husika kwa Maelezo zaidi
 
Ndugu,

Zingatia hapo kwenye swali lako nililobold, ndio ni vyema kuanza kwa kufuata taratibu zilizoainishwa pale kwenye kiambatanisho cha awali kwani kwa Tanzania ndio itakuwa INAANZA. Sasa kwa kuwa ni tumeshakuwekea mawasiliano ya wadau wanaohusika na mchakato huo basi ni vyema ungewasiliana na mamlaka husika kwa Maelezo zaidi.

Lakini kama nilivyokueleza awali Taasisi hizi husajiliwa chini ya sheria tofauti tofauti kama vile Sheria ya Vyama, Sura 337, Sheria ya Udhamini, Sura 375 na Sheria ya Makampuni, Sura 212/213. Sasa kwa kuwa hatuna ufahamu wa muundo na malengo ya shirika lenu inatuwia vigumu sana kuwashauri ipasavyo, hata hivyo, tunaweza kuwapatia picha kidogo, (na hapa tutaassume kuwa awali Taasisi yenu ilisajiliwa kama NGO lakini yenye muundo wa Kampuni)

Usajili
Inakupaswa uelewe kuwa kuna mashirika Makubwa ya Kimataifa yaliyosajiliwa kama NGO huko kwao, lakini yana hadhi ya kampuni lisilokuwa na mtaji, yaani Company Limited by Guarantee, not having a share capital
Sasa ili Shirika kama hilo liweze kufanya Shughuli zake kihalali hapa Tanzania ni lazima kwanza likidhi matakwa ya Sheria ya Makampuni (The Companies Act Cap 212), yaan lisajiliwe kwa mujibu wa part XII of Cap.212 kwa kuwa awali lilisajiliwa nje ya Tanzania

Foreign companies (companies incorporated out of Tanzania)
# These are companies incorporated outside Tanzania. Their offices in Tanzania are treated as branches of foreign company. They are registered under part XII of Cap.212
# The Registration procedure of this type of companies include the submission of :-
>Certified copies of Memorandum and Articles of Association.
>Notice of the location of the registered office in the country of domicile.
>List of Directors of the company.
>Persons resident in the country who are the representatives of the company

Baada ya kupata hiyo certificate kutoka BRELA ndio unakwenda kwa Registrar of NGO kuomba Cheti cha Ukubalifu (Certificate of Compliance) kama ilivyoelekezwa kwenye kile kiambatanisho cha awali.

Ukitaka Ushauri wa Uhakika ni vyema ukawa muwazi, kwa kutupatia taarifa sahihi na zilizojitosheleza. Lakini kutokana na suala la kiusalama na usiri ni vyema ukawasiliana na Taasisi husika kwa Maelezo zaidi

Mkuu asante sana kwa ushauri na maelezo ya kina . Godbless.
 
Back
Top Bottom