Msaada kuhusu biashara ya kinyozi mkoa wa morogoro

Msaada kuhusu biashara ya kinyozi mkoa wa morogoro

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Wanajamvi salaam,

Nina mpango wa kufungua biashara ya saloon (kinyozi) mkoani morogoro. Kwa wenyeji wa morogoro nahitaji kupata uzoefu wenu kwenye hili katika mambo yafuatayo;

Mosi, ni maeneo gani kwa mkoa wa morogoro biashara hii itachanganya au itafaa kuanzishwa?

Pili, Vipi gharama za kunyoa kwa mkoa wa morogoro ni shilingi ngapi kwa mtu mmoja?

Tatu, je kwa kawaida makubaliano kati ya mwenye kinyozi na wanaonyoa huwa yanakuwaje?

Mwisho, bei ya frem na upatikanaji wake ukoje kwa mkoa wa morogoro?

Natanguliza Shukurani zangu kwa wote mtakaotoa maoni.
 
Hii biashara cjawah kuipenda
Cjui kwann Ila all the best mkuu
Ufanikiwe

Japo mawazo yang n kufungua saloon
Ya kinadada
 
Umefatilia bei y'a machine Za kudumu na bei ya Kioo Kwa mita?
 
Fungua mitaa ya pale mjini karibu na CRDB iwe ya kisasa utapata wateja wengi. Ila iwe ya kisasa na hudum bora kwa wateja.
 
Mada za kitoto hizi. Haingii akilini dume zima kuileta hapa.
 
Back
Top Bottom