Msaada: Kuhusu Biashara ya kuuza mchele jumla kutoa mikoani kuleta Dar

Msaada: Kuhusu Biashara ya kuuza mchele jumla kutoa mikoani kuleta Dar

Procurer

New Member
Joined
Jan 3, 2021
Posts
4
Reaction score
3
Habari Ndugu zangu,
Napatikana Dar es Salaam nahitaji kuanza biashara ya kununua mchele kutoa mikoani kuleta kuuza jumla DSM, hivyo naombeni msaada kwa mwenye uzoefu wowote na biashara hii ili nami kijana mwenzenu nipate kujiajiri katika biashara hii.

Nina mtaji wa chini ya million 5, sijawahi kufanya biashara hii ndio nahitaji kuanza.

Nahitaji kujua ;-
1. Kuhusu upatikanaji wa mchele?
2. Gharama za kununulia
3. Gharama za usafirishaji
4. Misimu ya ununuzi wa mchele
5. Upatikanaji wa masoko
6. Kuhusu Gharama nyingine zozote zinahusika ikiwemo Ushuru na n.k
7. Mengineyo yanayohusiana na biashara hii.

Natanguliza shukrani zangu kwa wote mtakao ungana na mimi kutoa michango yenu ya mawazo.
 
Mchele kwa sasa jijini Dar es salaam unakwenda Tsh ngapi kwa kilo 1?
 
Mchele unao uzwa dar mala nyingi utokea mbaya kiela Ifakara Morogoro na kahama isaka kagongwa hizi sehemu ziko shinyanga

Sehemu ya kuuzia dar tandika mbaghara na tegeta kwa ndevu na Tandale lakini kwenye uhakika wa soko ni tandika temeke sababu tandika kuna magodauni ya Wapemba na wasukuma ukishusha mchele wako kwao wanauza kisha wanakupa hela yako malipo yao sh 100 kwa klo kuhusu uaminifu usihofu

Shinyanga kuna mchele mzuli pamoja na mbeya ila bei yao kubwa kuliko Morogoro lakini usafiri rahisi

Morogoro mchele wake bei chini ila usafiri uko juu sababu ya njia mbovu Ifakara marinyi mlimba nyia mbovu lakini mchele wao bei chini ila sio bora kama huko mbeya na kahama

Tani 1 kutoka Ifakara dar 110
Kahama dar tani 1 sh 80 mpaka dar mbeya hivio hivio

Ushuru Ifakara kl 100 3000/
Kibega kupakia 1000 kushusha 1000
Mfuko 1000 kujaza mchele kwenye mfuko pamoja na kupakaza mafuta na kununua hayo mafuta sh 3000 kwa kl 100

Kwa bei ya leo mchele bei ya jumla mashineni sh 2600 kwa klo mauzo dar sh 2900 mpaka 2850 kwa klo

Kokotoa hesabu hizo utajua unanunua vipi na kuuza vipi na wapi pa kuuzia kama ujaelewa vizuli jiulize nikufahamishe zaidi
 
Back
Top Bottom