Msaada kuhusu Haki za Madereva Barabarani

silver25

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
743
Reaction score
44
Wana jukwaa la Sheria, naomba msaada wenu

Ni wiki Tatu sasa tokea Askari mmoja pale Tegeta kwa ndevu, kituoni kuninyang'anya Leseni yangu. na amekuwa akinizungusha kunipatia kwa kigezo cha kwamba nikimlazimisha sana atakipeleka kwa RCO ili aifute Leseni hiyo.

Nimekuwa nikiwaza na kuwazua, nijue sheria aliyoitumia Askali huyo ambaye muda wte namkuta amelewa Pombe ili na mimi niweze kumkamata kwenye sheria nimekosa.

Scenario ilikuwa hivi, Alinikamata baada ya kupiga uturn sehemu ambayo anadai haikuruhusiwa, lakini kibao cha no uturn hakikuwepo, hivyo nikamwambia anioneshe alama ya no uturn na kuniambia hilo si kosa bali yeye anataka kunikagua, nikampa Leseni, akaaikagua na kuondoka nayo, kisha hapo ndipo yakatokea mabishano ya yeye anirudishie leseni niendelee na safari wakati yeye anasema anasubiri tuelewane.
 
Hana lolote huyo anataka rushwa tu mimi naona bora ukamripoti mapema km kesi imuangukie yéyé na rushwa usimpe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…