Msaada kuhusu kipimo hiki cha matatizo yote ya mwilini

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Wanajf ninaomba anayekifahamu kipimo hiki anieleweshe!Ni kipimo nimeambiwa unalipia sh.30000,wewe ni kukaa na kusubiria majibu ndani ya dakika chache!Utaambiwa shida zako zote!Kwa kuwa ni suala la kiafya ninaomba wataalamu njooni mnielimishe kwani kama mnavyojua sasa hivi "afya" imegeuzwa ni biashara kwa baadhi ya watu!Ninaomba mnaponijibu mnielimishe ubora na usahihi wa kipimo hicho maana kwa uelewa wangu huu kiduchu naona kama kinatumia mionzi ingawa sina uhakika!!MSAADA TAFADHALI NIMEAMBATANISHA NA PICHA
 
Attachments

  • KIPIMO CHA MWILI MZIMA.jpg
    KIPIMO CHA MWILI MZIMA.jpg
    77.9 KB · Views: 7
Wanajf ninaomba anayekifahamu kipimo hiki anieleweshe!Ni kipimo nimeambiwa unalipia sh.30000,wewe ni kukaa na kusubiria majibu ndani ya dakika chache!Utaambiwa shida zako zote!Kwa kuwa ni suala la kiafya ninaomba wataalamu njooni mnielimishe kwani kama mnavyojua sasa hivi "afya" imegeuzwa ni biashara kwa baadhi ya watu!Ninaomba mnaponijibu mnielimishe ubora na usahihi wa kipimo hicho maana kwa uelewa wangu huu kiduchu naona kama kinatumia mionzi ingawa sina uhakika!!MSAADA TAFADHALI NIMEAMBATANISHA NA PICHA

Hakuna kipimo cha mwili mzima, bali kuna vipimo mbalimbali vinavyoweza kufanywa kimoja kimoja au vyote kwa pamoja ili kuweza kubaini ugonjwa.

Kuwa makini. Kama watu wamebuni mitambo yao basi usikimbilie tu kutumia au kutumika kama sehemu ya kufanya majaribio ya mitambo/mashine hizo. Hizo mashine zimethibitishwa kuwa salama kupima au zinatoa majibu ya ukweli?

Nafikiri kama hivyo vipimo au vifaa vipo basi serikali kupitia wizara ya afya na mamlaka zingine wangethibitisha uwepo wake na hata kupatikana katika vituo vya afya na hospitali.

Ukiwa na shida ya kiafya ni vyema ukafika katika kituo cha afya kinachotambulika rasmi uonane na daktari uhudumiwe kisawasawa.

Kila la kheri.
 
Waongo hao.
 
Tatizo ni kwamba hawa watu wako nchini wanafanya kazi!Swali mbona wizara ya afya iko kimya??
 
Back
Top Bottom