Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli ina uchakavu..ila dumping fee isikusumbue kama gari umelipenda huyo mchangiaji hapo juu kakuuliza mambo ya cc na aina ya gari lilikuwa swali zuri maana ukijumlisha na cif ungewezajua gharama za uchakavu...gari la mwaka 2003 lina uchakavu lakini TRA wanawezakubali kuwa CIF yake ni $2500 lakini gari la 2005 halina uchakavu na TRA hawatakubali kuwa CIF yake ni $2500 watasogeza juu (uplift)na kuwa $3200 sasa japo huyu hatalipa uchakavu lakini anawezalipa kodi ya juu au sawa na wewe unayelipia uchakavu..sasa unachotakiwa kufanya kama umelipenda lichukue agent wako anaweza kuweka CIF ya chini..hesabu ikawa chini
gari yako ina
1.cc ngapi?
2.aina ya gari-model yake?
3.mwaka-2003-ok
Mkuu samahani sana, kutokana na ushauri wa mdau lucky sababa nadhani ulitaka kushauri zaidi, I thought you overlooked!
Ni Suzuki Swift, ina cc 1300, ni ya mwaka 2003, CIF value USD 2,166
Tatizo hilo la mito hatujui ni rangi gani..katika ununuzi wa magari rangi na mwaka wa kutengenezwa vinapanga sana bei..hili lililoonyeshwa hapa ni jeupe lakini hilohilo lingekuwa silver au maroon bei yake ingepaa sana plus inspection,local charges na shipping litakuja bei hiyo hiyo ya mito...siku zote in vehicle biz rangi nyeupe ni cheap,na ata linapogongwa kulipiga rangi hiyo ni cheaper si kama nyingineFoB yake ni kiasi gani? Kuna nyingine hii hapa bei poa kabisa ya mwaka huo huoSuzuki Swift UA-HT51S(2004) / SE-Z#
Tatizo hilo la mito hatujui ni rangi gani..katika ununuzi wa magari rangi na mwaka wa kutengenezwa vinapanga sana bei..hili lililoonyeshwa hapa ni jeupe lakini hilohilo lingekuwa silver au maroon bei yake ingepaa sana plus inspection,local charges na shipping litakuja bei hiyo hiyo ya mito...siku zote in vehicle biz rangi nyeupe ni cheap,na ata linapogongwa kulipiga rangi hiyo ni cheaper si kama nyingine
Wakuu kuna gari nimeipenda, ila ni ya mwaka 2003, wasiwasi wangu ni je ina kodi ya uchakavu? nimepitia nyuzi za magari pamoja na website ya tra lakini sijaelewa namna tra wanavyohesabu hiyo miaka 10 yao. Naomba mwenye uzoefu anijuze tafadhali
Gharma kamili ni Tsh 2,705,666. ama ni $1.691
Usitishwe na uchakavu bali angalia engine size na spare parts availability hapo bongo. Ukitaka msaada zaidi ni PM nitakupa maelezo zaidi. Nina uzoefu mkubwa sana na haya mambo.
Unaweza kupiga simu TRA customer service utahakikisha ninachokueleza.
Hii ni kweli kabisa ndio maana nimemwambia bwana mito aandae 3+++ml kwa ajiri ya ushuru,kabda ya mambo ya online purchasing bei za magari zilikuwa zinaeleweka vizuri siku hizi hazieleweki,ndio maana TRA wanabase zaidi na CIF zao..unajua hapa duniani soko kubwa kuliko yote ya used cars za mkono wa kulia lipo dubai linaitwa Al aweer used auto market(waweza ku google ukapata habari zaidi)kipindi watu walipokuwawananunua magari kule bei zilikuwa zinaeleweka,sasa siku hizi na hizi teknolojia watu wa pakistani na wahindi(hawa ndio wameshikilia soko la magari dubai na japan) wanakwenda japani mnadani na kuuza magari online,bei zinakuwa hazieleweki maana pale ni mkusanyiko wa magari mengi mengine yamepata ajari mengine ya deal nk,sasa ni ngumu sana kwa TRA ku base na CIF zinazotoka kwa wateja..wao wanabase na CIF ya showroom na ukizifuatilia CIF za tra zipo sahihiWakuu CIF siku hizi wanapanga TRA wenyewe na kuna bei wameshaziweka kabisa ya gari ikiwa mpya then wana calculate depreciation kutokana na miaka ya gari yako so CIF value unayowapa haina kazi wao ndo wanakupa CIF mimi nilinunua VW CIF ilikuwa 2300 lakini wao wakaniambia ni 3500