Msaada kuhusu kubadilisha ngazi ya utumishi serikalini

Msaada kuhusu kubadilisha ngazi ya utumishi serikalini

YAHAY

Member
Joined
Apr 28, 2012
Posts
11
Reaction score
0
Habari wana jamii forum, ni matumaini yangu mambo yanenda sawia.

" Kwa taratibu ambazo zilikuwepo awali ni kwamba mtumishi wa serikali akijiendeleza kimasomo katika taaluma anayoifanyia kazi anaporudi kwa muajiri wake humpandisha ngazi ya utumishi ambapo mtumishi anahitajika kuonesha vyeti vyake alivyovipata baada ya kuhitimu hiyo taaluma yake SWALI LANGU NI KUWA kwa upande wa walimu mtu ukishajiendeleza mfano kwa level ya digrii utahitajika kuonesha Transcrits ili wakupandishe kuwa level uliyosomea, SASA WAKUBWA mimi ni mwalimu niliyejiendeleza kozi ya digree in education, niliporudi Kwa mkurugenzi wangu WILAYA YA KILOMBERO kwa ajili ya kuapgrade mshahara wangu ili nilipoti kituoni kwangu wananiambia kuwa Hawapokei Transcript ya matokeo peke yake bali wanataka na cheti cha chuo Je? utaratibu huu ni kwa wilaya zote nchini au umakumashi ambao upo katika wilaya hii? Isitoshe walimu wapya wanaajiriwa na Transcripts hizohizo kwani vyeti vinatolewa navyuo baada ya mwaka mmoja kumaliza, mfano mimi nimesoma Udsm. Hivi kweli inaingia akilini mimi nikae Mwaka mzima nisubirie Cheti hali ya kuwa wale niliomalizanao chuo wameajiriwaq kwa Transcripts zao na mimi mwajiriwa wa serikali hiyo hiyo nisubiri baada ya mwaka mmoja nitakapo pata cheti ndo wanilekebishie mshahara wangu. WADAU NAOMBENI MAJIBU KWELI UTARATIBU NDO UKO HIVI NCHI NZIMA?
 
Wewe hujajua shida yao nyoosha mikono wewe umeikunja 2, fanya hvyo fasta uone
 
Ukweli hata Wilaya yangu hawabadilishi muundo bila cheti. Wweza nyoosha mkono lakini wakituma data zako utumishi bila cheti zitatupwa kenye jalala la utumishi na tsd anaweza pata kweri ya kujibu. Kuwa mpole,vumilia cheti kitoke then watakubadilishia muundo. Labda hapa kuna haja ya kuashauri viongozi wa udsm watoe vyeti haraka,mbona out wanatoa haraka,ndani ya mwezi unakipata kama ukimaliza kila kitu,yaani umefaulu na ada umelipa.
 
Mimi niko wilaya ya kinondoni, nilimkuta mtumishi poa sana, alichoniambia ataupload data zangu pamoja na hiyo transcript ingawa utumishi wanataka cheti, akasema tujaribu kama try and error, wakireject basi. Ilikuwa tar 9 may kufika tar30 mshahara mpya teari. So ni suala la wanaupload hizo dat a. Nenda utumishi kaeleze shida yako
 
wengine wanakuwa na bifu za kijinga, wkt mwingine bifu tunaishi nazo bila kujua, transcrpt inatosha sana wakuu, pia angalia umewatukana hapo bila kujua!

Aisee mkubwa kweli nimetoa neno ambalo si la busara, unajua wakati mwingine uzembe ambao unatendeka na watendaji wa serikali yetu unatia hasira sana, any way ilikuwa nataka nipate majibu tu, nashukuru sana wadau.
 
Back
Top Bottom