MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,607
Kwanza nenda kuitaarifu polisi kuhusu hicho kisago unachopata, wao watakupa fomu ya hospitali na mahakamani. Pia Ustawi wa jamii, TAMWA wako makini na unyanyasaji wa kijinsia. Watakuunga mkono na kukusaidia.
Tukubali kuwa wanaume wengine (na wanawake wapo ingawa ni kidogo kuliko wanaume) ni maafande katika ndoa zao, wanapiga na wanatesa kimwili na kiakili. Mimi sidhani kama Mungu yuko na watu wa aina hii eti kwa sababu ya ndoa. Kama alivyosema mmoja wetu, ndoa ni makubaliano ya wawili, mmoja akienda kinyume na makubaliano hayo, hamna ndoa, tabu ni kuwa mmoja au nyote mnapoamua kuvunja mkataba huo ndio tena wanatokea wapambe, sijui mahakama, sijui padri. Dada, ikiwa ankutesa, iwe Mtanzania iwe Mchina, hastahiki kupewa hadhi ya mume.
"Wanaotesa wanawake ni waoga na wana matatizo ya kisaikolojia".