Msaada kuhusu mdogo wangu asome course ipi.

Msaada kuhusu mdogo wangu asome course ipi.

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
1,739
Reaction score
748
Katika familia yangu mimi ni wa kwanza na jumla tupo watano. Na mama yetu ndo aliyetulea mpka kufikia hapa.
Mimi nimesoma na ni Daktari wa binadamu yaani MD.
Mdogo wangu aliyenifuata amesoma Mv mechanics mpka grade 1 kwa level ya VETA.
Mdogo wangu wa 3 yeye ni mwanafunzi wa udaktari MD mwaka wa 3 sasa anasoma miongoni mwa vyuo vya afya hapa bongo.
Wadogo zangu wa mwisho ni mapacha wao wako secondary form3. Mmoja anauwezo sana ambapo kwa mtazamo wangu kama mambo yakienda vema naamini atafaulu, huyu mwingine uwezo wake ni wa kati. Sasa concern yangu ni huyu mdogo wangu ambaye anauwezo mzuri sana darasani, yeye anainterest ya kusomea udaktari lakini mimi sijapenda sana coz haiwezekani familia zima tuwe madaktari. Sasa naombeni ushauri asome course ipi ambayo iko na market na ambayo itatuunganisha familia. Najua kila moja kufuata ile moyo inapenda huwa ni vizuri zaidi lakini pia kuweka famila ambayo inaprofessional nyingi mnakuwa uwanja mpana wa kufanya mambo makubwa. Msaada plz.
 
Back
Top Bottom