Msaada kuhusu mkopo wa vijana Halmashauri

Mr connecter

Member
Joined
Jul 13, 2023
Posts
16
Reaction score
4
MSAADA WA KUFAMU JAMBO KUHUSU MKOPO WA SELIKALI

Habali wanandugu;
Mimi ni kijana wa makamo naomba kuuliza jambo. Huwa nimesikia kuwa katika hii nchi yetu huwa inatoa mkopo kwa vijana kwa wajasilia Mali na wakulima vijana na fungu hilo lipo katika bajeti ya serikali na hupelekwa kwa kila mkoa katika halmashauli zake.

Sasa naomba kuuliza utaratibu wake unakuwaje na unaanzia wapi na vigezo vyake ni vipi na unakopa kwa muda gani na kiasi chake ni kipi na je una riba?

Msaada wenu nduguzangu🙏🙏🙏
 
Uwa ni 10% ya mapato ya halmashauri yanatengwa kwa ajili ya mkopo ambao hauna riba kwa vijana, wanawake na walemavu, hili kuweza kupata mkopo lazima muwe kikundi cha watu 5-10 na wazo la biashara pia umri kwa wanaume ni chini ya miaka 35 kama sijakosea hila wanawake akuna limit ya umri, ili kuweza kupata nenda ofisi za kata muone afisa maendeleo atakupa maelezo na utaratibu wa jinsi ya kupata mkopo hiyo
 
Nashukulu kiongozi kwa mchanganuo huo , mkopo huu apewi mtu mmoja pekeyake mpaka kiwe kikundi tu pekeyake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…