Msaada kuhusu Mtoto kutokucheza tumboni wakati wa ujauzito

musajohn58

Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
34
Reaction score
8
Imetokea kwa binti mwenye ujauzito wa miezi saba mtoto akaacha tu kucheza pasipo sababu takribani siku tano sasa, ila kipindi cha nyuma alikuwa anaumwa tumbo sana akafanyiwa uchunguzi hospital ikaonekana na UTI,

Je hilo tatizo la mtoto kusimama tu kucheza huwa kunashida??

Alienda kupima ikaonekana mapigo ya mtoto yako kwa mbali sana. Sababu ya mapigo kuwa kwa mbali huwa ni nini?
 
Huyo anaitaji njumu na mpira meza halafu leta mrejesho
 
Kwa mazingira ya kawaida huo muda wa siku tano ulizozitaja ni mrefu sana mtoto kutocheza kwa jinsi ninavyofahamu.., ukichukulia ukubwa wa mimba..!!)))
Huyo aliyempima na kukuta mapigo yapo chini sana na kumruhusu arudi nyumbani bila kumlaza kwa uchunguzi zaidi sijajua alikuwa na sababu zipi zaidi kufikia uamuzi huo...!!!)))
Sababu zipo nyingi sana zinazoweza pelekea mtoto kutocheza.., nyingi si nzuri ukiondoa ile ya kwamba mtoto anaweza kuwa amelala(Ila si siku tano mfululizo.., watoto huwa wanalala mda mrefu zaidi kuliko mda wanaokuwa macho.., ie zaidi ya masaa 16 ila ni ndani ya mzunguko wa masaa 24).
Kama mimba ni ya kwanza kwa wengine inaweza kuwa ngumu kusikia mtoto akicheza hasahasa ikiwa mtoto anacheza usiku(ie mama akiwa amelala)..!!)))

USHAURI
Aende clinic inayoeleweka aombe kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama(ie OBSTETRIC GYNAECOLOGIST) kwa msaada wa kitaalam...!!!)))
 
Asante sana kwa ushauri wako mzuri, hii sio ishara nzuri hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…