Msaada kuhusu mzunguko wa hedhi

Msaada kuhusu mzunguko wa hedhi

chikuyu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2013
Posts
277
Reaction score
179
Naombeni Msaada,
Mke wangu alitumia hivi vidonge vya uzazi wa mpango, baadaye akaamua kuachana navyo baada ya kusikia kuwa vina madhara yake pia.
Sasa changamoto imekuja kwenye mzunguko wa hedhi; umevurugika, Kwa mfano, kwa mara ya mwisho mzunguko ulianza tarehe 7 July 2016, halafu mzunguko mwingine ukaanza tena juzi tarehe 22 July. Sasa tumeshindwa kuelewa ni nini tatizo?
Hospitali tumeenda huko, kuna nesi akatupatia vidonge kwamba vitarekebisha huo mzunguko, kumbe vidonge vyenyewe vikaonekana ndo vile vile vya uzazi wa mpango alivyopewa mwanzoni, sikumbuki jina ila ni vidogo hivi unameza kwa kwa muda wa miezi mitatu kimoja kila siku!!
Naombeni msaada wenu wataalaam!!
 
Kama vinafanana na vya uzaz wa mpango ni dawa iyo...... Pia niliwah tumia vikanitibu...... But jina nimesahau kidogo...
 
OK dada, na wewe ulikuwa na tatizo kama hilo hilo?
 
Hii tatizo hata mchumba wangu ana miezi miwili hajaona siku zake na kila akipima mimba hana je tatizo lipo wapi wana jf
 
Dawa zote za uzazi wa mpango ni shidaa zinamadhara na karaa kama hio so kuna makini sana pia jifunzeni kutumia karenda utaenjoysana
 
Dawa zote za uzazi wa mpango ni shidaa zinamadhara na karaa kama hio so kuna makini sana pia jifunzeni kutumia karenda utaenjoysana
Numekupenda bure kwa text yako hii hasa hapo mwisho watu watumie kalenda tatizo watu ni wavivu kujifunza ni wakati gani mimba inatungwa na wakati gani mimba haitungwi
 
Back
Top Bottom