Msaada kuhusu nauli za ndege

Cod-2

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2017
Posts
297
Reaction score
434
Habari wakuu.

Nimekuja kwenu kuomba msaada wa nauli ya ndege kutoka bukoba kuja dar (one way)

Ieleweke kwamba Mimi sijawai panda ndege, kuna binti nahishi naye sasa alipata ujauzito ikabidi nimpeleke Kwa mama kijijini akajifungulie kule kutoka na shughuli za mjini asingeweza pata huduma nzuri baada ya uzazi. MUNGU mwema kajifungua salama mwezi wa tano mwanzoni.

Kwa ufupi nilipanga kumkatia tiket ya ndege wakat wa kurudi huku na mtoto. Nataka arud. mwez wa 7 mwishoni,
kwahiyo nilkuwa naomba mwenye Link au anayejua nauli na namba nzima ya booking anisaidie, maana nilisikia uki-book mapema Kuna punguzo kidogo kwenye nauli.

Asante

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mimi mara ya kwanza na mwisho nilipanda ndege kwa Tsh 57,000 tu sijui labda sasa hivi imefikia elfu 70 sijui maana imepita miaka 10
 
Haya fanya fasta utuongezee mapato. Welcome on board ......

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…