JMF
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 1,758
- 2,770
Salaam wana jukwaa,
Kuna eneo(kiwanja) nahitaji kununua sehemu. Ila ni kama kuna utata kuwa ni kwaajili ya makazi au biashara au yamkini ni eneo la serikali kwasababu kipo karibu na eneo la soko. Hivyo nikaona ni bora nitafute taarifa za eneo husika nisijekuingia mkenge.
Nawezaje kupata taarifa sahihi? Nimefuatilia hadi ofisi za kata lakini ni kama wananena kwa lugha tofauti. Wapo wanaosema ni kwaajili ya makazi, biashara, ni eneo lililotengwa kwaajili ya upanuzi wa soko na wakazi waliopo wanawezalipwa fidia waondoke. Wapo wanaosema upanuzi wa soko haufiki huko hivyo nikaona nililete hapa kwa msaada zaidi na ushauri