Msaada Kuhusu Shughuli Za UTT Amis

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,200
Reaction score
12,762
Naomba kufahamishwa shughuli za shirika hili hasa katika mambo ya fedha na namna ya kuweka fedha na kupata faida.

Maana katika hali ya Sasa utapeli umekuwa ni mkubwa Sana hivyo ni bora kupata a,b,c,d kuhusu shirika hili kabla mtu hauja ingia kichwa kichwa kuweka fedha na mwisho ukaliwa kichwa uku ukiwa na malengo ya kupata faida.
 
Ila UTT ni bonge la mchongo mwaka jana nimevunja kibubu changu cha chuma nikakuta m8 na usheee pesa nilijibanabana mwenyewe hamna kilichoongezaka, mwaka huu 15/05/2022 nikafungua account UTT nilianza na laki 5 na baada ya hapo nikaendelea na utaratibu kama naweka kwenye kibubu nikipata 10k au 20 naweka kulingana na harakati zitakavyokua mpaka muda huu kuna ongezeko la sh 5117 pesa ambayo ningeweka kwenye kibubu nisingeipata hata buku wadau kama itakupendeza ifanye UTT AMIS iwe kibubu chako
 
Hakuna changamoto zozote za kuweka pesa uko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…