rama halavi
JF-Expert Member
- Nov 20, 2015
- 269
- 236
Habari za wikiend? Natumai wadau wote JF katika sekta hii mko poa, Mimi ni mgeni katika jukwaa hili japo nimekuwa nikipita mara kwa mara kujifunza kitu kipya katika maswala ya uchumi na biashara coz mi mwenyewe ni mjasiriamali na mfanyabiashara. Mwaka jana mwezi wa 9 nilienda TRA kuomba TIN namba na walipiga hesabu zao kuhusu biashara yangu na kodi stahiki ninayopaswa kulipa na nikaenda benki kulipa, niliporudi wakati napewa TIN Namba yangu niliambiwa nirudi tena mwezi wa pili ila nilisahau kuuliza kwanini, sasa huu ni mwezi wa pili na ghafla nikakumbuka kuhusu hili ndio maana nikaamua kuomba msaada.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu nahitaji msaada kuhusu maswala ya TIN namba. Maswali yangu ni kama yafuatayo:
a) Je TIN namba huwa inalipiwa kila mwaka au ukishukuwa nayo hamna tena malipo?
b) Je unaweza kutumia TIN namba yako kwa ajili ya biashara tofauti? mf: (duka na pikipiki)
Natumai wenye ufahamu zaidi watanisaidia katika hili. Ntashukuru nikipata feedback