Msaada kuhusu TIN namba

Msaada kuhusu TIN namba

rama halavi

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2015
Posts
269
Reaction score
236
Habari za wikiend? Natumai wadau wote JF katika sekta hii mko poa, Mimi ni mgeni katika jukwaa hili japo nimekuwa nikipita mara kwa mara kujifunza kitu kipya katika maswala ya uchumi na biashara coz mi mwenyewe ni mjasiriamali na mfanyabiashara. Mwaka jana mwezi wa 9 nilienda TRA kuomba TIN namba na walipiga hesabu zao kuhusu biashara yangu na kodi stahiki ninayopaswa kulipa na nikaenda benki kulipa, niliporudi wakati napewa TIN Namba yangu niliambiwa nirudi tena mwezi wa pili ila nilisahau kuuliza kwanini, sasa huu ni mwezi wa pili na ghafla nikakumbuka kuhusu hili ndio maana nikaamua kuomba msaada.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu nahitaji msaada kuhusu maswala ya TIN namba. Maswali yangu ni kama yafuatayo:

a) Je TIN namba huwa inalipiwa kila mwaka au ukishukuwa nayo hamna tena malipo?

b) Je unaweza kutumia TIN namba yako kwa ajili ya biashara tofauti? mf: (duka na pikipiki)

Natumai wenye ufahamu zaidi watanisaidia katika hili. Ntashukuru nikipata feedback
 
Nitajaribu kukujibu ninavyofahamu mimi kafiri ya upeo wa ufahamu wangu.

a) Unacholipia ni income tax yaani ni kodi ya mapato ambayo ni 20% ya faida yako kwa mwaka, kinadharia. Lakini kihalisia wafanyabiashara wingi hulipia chini ya hapa pengine 1-2% kwa vile hakuna anayekuwa mkweli katika kusema anapata faida kiasi gani. TIN, Taxpayers Identification Number, ni nambari ya utambulisho wako tu huko TRA ni sawa na jina lako kwa wazee, hailipiwi.

b) Unaweza kutumia hiyo TIN number kwa biashara nyengine, kwa sharti ya kwamba uwajuilishe TRA ili wafanye makadirio mapya. Biashara iwe na uwiano kwa mfano kama kule mwanzo TIN number yako ni mjasiria mali, huwezi kuitumia TIN number hii kwa partnership ama Limited Company. Lakini watu wingi huamua kuwa na TIN number tofauti kwa biashara tofauti kwa sababu zao binafsi tu. Ninavyojuwa mimi unapojaza fomu ya marejesho, unataja njia zote za mapato yako kwa TIN number hiyo hiyo kwa ajili ya kufanyiwa hesabu za kodi.

Natumai imekufunuwa ubongo kidogo
 
Back
Top Bottom