Tatizo jingine tulilonalo ni ubabaishaji kwenye kodi zetu leo utaagiza hiki kodi utatoa hii kesho utaagiza kilekile kodi inakuwa tofauti sana,kuna mwaka niliagiza gari tax ikaja 4.6ml nakumbuka nilikwenda pale Tra karibia na central police ghorofa la kwanza kuna ofisi imeandikwa Vehicle ....niliongea na yule mzee nilishangaa alinipunguzia almost 1.5ml!!!system yetu ya kodi haieleweki
Ndiyo maana siku zote nasema
kama unataka gari,nenda show room ya magari,tafuat gari unalotaka,unalina,limelipiwa ushuru,nunua gari,ondoka zako,hii presha ya bandari na TRA unashuka uzito kila saa tangu umeagiza china!
Ebwana shipping agent mara ya mwisho baada ya kuambiwa alichofanya si sahihi alirudi TRA kuangalia uwezekano wa kufanya appeal lakini mpaka sasa hakuna mawasiliano na agent kwani hapokei simu, hajibu sms, yaani hakuna kinachoendelea zaidi ya kusema kwamba nikikamilisha nitakujulisha......
Hapo kazi ipo, kwa hiyo docs ziko mikononi mwa agent na hapokei simu? Ni siku ya ngapi sasa? Tatizo la maagent wa kibongo wanafanya kazi kiswahili sana, hawana uwazi, na wakiona unawapigia sana wanakuwa hawapokei simu kukupa updates!