Msaada kuhusu ugonjwa wa asma

Msaada kuhusu ugonjwa wa asma

Landala

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2010
Posts
997
Reaction score
478
Jamani naombeni msaada kuhusu ugonjwa wa athma,chanzo chake ni nini na je mtu akiugua anaweza kupona.
 

Pumu, Kuvimba mapafu na Kuziba Pua


Tunapopumua, hewa huvutwa ndani ya mapafu wakati kiwambo (diaphragm), ambacho ni mfupa kinapokuwa kimejikaza kikivuta chini, kikiondoka kutoka chini ya mapafu na kutengeneza chumba ili mapafu yatanuke.

Mwendo huu hutengeneza uwazi katika mapafu yote, ukiyajaza hewa mapafu. Wakati kiwambo kinasinyaa huchupa nyuma juu kikisukuma hewa nje ya mapafu.

Hewa huingilia puani ambako huchujwa na kupashwa joto au kupitia mdomoni wakati pumzi nzito imehitajika.
Kwenye mzizi (nyuma) ya ulimi kuna kifuniko (valvu) kimetengenezwa kwa katileji iitwayo kidakatonge (kimio). Hiki ni kifuniko kinacholinda kisanduku cha sauti (larynx) ambamo bomba la upepo (trachea) ambalo ni tyubu kubwa huanzia. Kifuniko hiki kitajifunga wakati unameza chakula au ukinywa kimiminika, pia hubaki wazi wakati ukipumua hewa ndani au nje.

Tyubu hiyo kubwa (bomba la upepo) kisha imegawanyika katika matawi mawili yaitwayo vikoromeo (Bronchials) vilivyojishikiza katika kila pafu.

Pafu la kulia limegawanyika katika sehemu tatu (lobes) wakati pafu la kushoto ni dogo kidogo na limegawanyika katika sehemu mbili (lobes). Madaktari wanaweza kuondoa sehemu moja na pafu bado linaweza kuendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kikoromeo (Bronchial) kisha kimegawanyika katika tyubu ndogondogo ziitwazo neli neva za umio (Bronchioles). Kilichojishikiza mwishoni mwa neli neva za umio ni mkusanyiko wa vifuko vya hewa viitwavyo Alveoli.

Kila kifuko cha hewa (alveoli) kimezungukwa na kapilari za damu ambamo ubadilishanaji wa hewa (Air exchange) hutokea. Upande mmoja wa kifuko cha hewa oksijeni huingizwa ndani ya damu na upande wa pili wa kifuko hicho hicho cha hewa, gesi chafu iitwayo kabonidayoksaidi hutolewa.

Kabonidayoksaidi ni taka toka katika seli zetu zinazounguza oksijeni na chakula na kutengeneza nguvu na kutuwezesha kuishi.
Vifuko hivi vya hewa (alveoli) lazima vibaki na unyevunyevu ili ubadilishanaji wa hewa uweze kufanyika. Vifuniko hivi havijazwi maji, bali kuta au usawa wake wa ndani lazima uwe na unyevunyevu ili ubadilishanaji wa hewa uweze kutokea.

Maji huzifunika sehemu za ndani za vifuko vya hewa na unyevunyevu huu (surface tension) unahitajika ili kuwezesha kabonidayoksaidi kutolewa nje. Unaweza kuuona unyevunyevu huu (fog) kwa kuhema juu ya miwani ya jua au kioo chako.

Unapoteza glasi nne (4) za maji kila masaa 24 kwa kupumua tu.

Kila seli ndani ya mwili huwa na maji na lazima iwe na maji ili kubaki katika afya. Damu yetu ina asilimia 94 ya maji, ubongo wetu una asilimia 85 za maji na ogani na tishu zingine zina asilimia 75 ya maji.

Maji mengi kuzidi mwilini ni hatari kama ilivyo kwa chumvi nyingi kuzidi mwilini. Lazima kuwe na usawa wa chumvi ili kuhimili ujazo sawa wa maji ndani na nje ya seli kwa mujibu wa dr.Batmanghelidj.

Mahospitalini madaktari hutoa dripu la maji la lita moja lenye gramu 9 za chumvi ndani yake.
Ikiwa mtu anakunywa maji mengi na hatumii chumvi ya kutosha, maji yatakimbia kwa haraka nje ya mwili hivyo kutokuzipa seli za mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo. Yanaweza pia kutoa nje ya mwili madini na vitamini mhimu.

Hakuna mtu amewahi kupewa dripu la maji matupu bila chumvi hospitalini. Wanasayansi, wanakemia na madaktari bado hawaelewi ni kwa namna gani chumvi huyeyuka ndani ya maji na kuendelea kuyafanya maji kuwa na uchumvi na uchumvi kama maji ya bahari.
Dr. Batmanghelidj ameandika vitabu sita akielezea umhimu wa maji na chumvi. Kitabu kimoja kinaitwa: Asthma, Allergies and Lupus. Kitabu hiki kinafafanua namna magonjwa ya kuvimba mapafu (Emphysema), pumu (asthma) na kuziba pua (chronic obstructive pulmonary disease) yanavyojitokeza mwilini wakati mtu anapokuwa hana maji ya kutosha mwilini na ubongo kuamua kutuma ujumbe kwa mapafu ukiyaagiza kuanza kubana matumizi ya maji.

Wakati mapafu yanaanza programu ya kubana matumizi ya maji yanaweza kuzarisha ute ute na makohozi na kurundika katika neli neva za umio ili kuibana njia ya kupitia hewa na hivyo maji machache yatoke nje kwa njia ya mvuke wakati tunapumua nje ndani.
Ute na makohozi hushikamana na hivyo kuendelea kubaki hapo, pia huwa na unyevunyevu ili kufanya tishu laini zisikauke, zisipate nyufa na kutokwa damu.

Watu wenye pumu/asthma hudhibiti hali zao kwa kumeza dawa kila siku na kutumia vipumuzi (inhalers) wakati neli neva umio (Bronchioles) zimejibana (draw up) na tishu za ndani zinapokuwa zimeumuka (swolen) zikibana zaidi njia ya kupitia hewa na kusababisha shambulio la maisha katika kupumua.

Kwa kawaida shambulio la maisha hutokea wakati unafanya mazoezi au muda mfupi baada ya kula. Kwanza kikohozi kikavu huanza, kisha kupumua kwa shida hufuatia (wheezing), kukifuatiwa na tishio la maisha ukihangaikia kupumua ikiwa kipumuzi (inhaler) hakikutumika.
Wakati unafanya mazoezi unapoteza maji kwa njia ya jasho (perspiring), na kupelekea mishipa kuhitaji maji zaidi. Upotevu huu wa ziada wa maji unaweza kupelekea mapafu kujifunga zaidi na kusababisha kifo ikiwa kipumuzi hakitachukuliwa kuzuia mapafu yasijifunge.
Wakati unakula, mwili wako huelekeza mtiririko wa damu katika utumbo mdogo sambamba na maji ya ziada yanayohitajika kukishughurikia chakula. Baadhi ya vyakula (vyakula vigumu) huhitaji maji zaidi ili kushughurikiwa (kumeng'enywa) kuliko vingine. kwa hiyo kama wewe unakula vyakula vigumu vigumu na una sumbuliwa na pumu/asthma basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa madhara yatokanayo na magonjwa haya yanakujia mara nyingi zaidi kuliko wengine.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji na umekula chakula kinachohitaji maji mengi ili kimeng'enywe, basi, mwili unaweza kukopa maji toka katika mapafu na kukusababishia shambulio la pumu mara tu kisha kula.

Inashauriwa kwa kila mtu mwenye pumu au kuvimba mapafu kunywa ml 250 (robo lita) za maji kabla ya kula chakula chochote na kunywa kiasi kidogo cha maji wakati ukiendelea kula chakula.

Dr. Batmanghelidj pia anasema watu wenye pumu wanaweza kuhitaji kiasi kidogo cha chumvi zaidi kwa muda ili kusafisha ute ute na makohozi mpaka mapafu yatakaporudi katika hali yake ya kawaida kama anavyofafanua katika kitabu: ABC of Asthma, Allergies and Lupus ukurasa wa 144.

Kamwe usinywe zaidi ya glasi mbili za juisi ya chungwa kwa siku ikiwa unasumbuliwa na pumu au una tatizo lolote katika mfumo wa upumuwaji. Kumbuka pia kutumia robotatu gramu za chumvi ya baharini katika kila robo lita ya juisi yako ya chungwa.

Haya ni mazingaombwe rahisi yanayohitaji kuongeza kiasi cha unywaji maji wakati mwili unapopungukiwa maji.

Dr.Batmanghelidj anasema; ‘hii ndiyo sababu pumu si kitu kingine zaidi ya upungufu wa maji mwilini, pumu si ugonjwa'.
Kabla ya kuamua lolote kuhusu tiba kwa kutumia maji, tafadhari soma vizuri: Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza tiba ya maji.
 
Nashukuru sana Fadhili Paulo kwa maelezo yako mazuri,je mtu mwenye ugonjwa wa pumu(asthma) anaweza kupona?
 
Nashukuru sana Fadhili Paulo kwa maelezo yako mazuri,je mtu mwenye ugonjwa wa pumu(asthma) anaweza kupona?

Ndiyo anaweza kupona kabisa, kwanini ishindikane?. Unaumwa mwenyewe au jamaa yako?
 
Ndiyo anaweza kupona kabisa, kwanini ishindikane?. Unaumwa mwenyewe au jamaa yako?

hapana sio mimi ila kuna mtu wangu wa karibu ndo alienda kupima akaambiwa anaumwa asthma lakini bado haijakomaa.
 
hapana sio mimi ila kuna mtu wangu wa karibu ndo alienda kupima akaambiwa anaumwa asthma lakini bado haijakomaa.

Nipatie urefu wake na uzito wake halafu tumponye asthma yake na kama alikuwa anadhani hawezi kupona basi utatuletea ushuhuda wake hapa akipona
 
Ndiyo anaweza kupona kabisa, kwanini ishindikane?. Unaumwa mwenyewe au jamaa yako?

Unaponaje? Mie wadogo zangu watatu wa kiume wote wanasumbuliwa na pumu tangu wamezaliwa wengine wanasema pia pumu huweza kupata kwa kurithi iwapo familia yupo mtu anaumwa...
 
Mmoja 20,15 na 7

urefu wake ni inchi 4 na uzito wake ni kg 55.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, pumu/asthma ni ishara ya mwili kupungukiwa maji na wala si ugonjwa.

Hatua ya kwanza katika kutibu pumu ni kuacha vinywaji au vyakula vinavyofanya maji kutumika zaidi au kutoka mwilini kwa haraka. Mgonjwa anashauriwa kuacha kabisa matumizi ya vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa na soda za aina zote kwa miezi kadhaa hadi atakapoona kabisa.

Ukibonyeza hapa kuna maelezo yote ya namna ya kutumia maji kujitibu na kila ugonjwa ikiwemo pumu, soma maelezo yote taratibu na uyaelewe penye swali niulize hapa hapa
 
Kama ilivyoelezwa hapo juu, pumu/asthma ni ishara ya mwili kupungukiwa maji na wala si ugonjwa.

Hatua ya kwanza katika kutibu pumu ni kuacha vinywaji au vyakula vinavyofanya maji kutumika zaidi au kutoka mwilini kwa haraka. Mgonjwa anashauriwa kuacha kabisa matumizi ya vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa na soda za aina zote kwa miezi kadhaa hadi atakapoona kabisa.

Ukibonyeza hapa kuna maelezo yote ya namna ya kutumia maji kujitibu na kila ugonjwa ikiwemo pumu, soma maelezo yote taratibu na uyaelewe penye swali niulize hapa hapa

Sawa shukraan sana...
 
Fadhili Paulo NAOMBA NIPATIE NAMBA YAKO KUNA NDUGU YANGU MWANAE ANASUMBULIWA SANA NA PUMU.ana miaka 6.uzito 20kg .usiku halali.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom