Msaada kuhusu Ujenzi kwa Mshahara huu

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
WanaJF,

Kabla sijaajiriwa kazini nilifanikiwa kujenga Pagara (Nyumba haijaezekwa). Sasa napokea Sh. 405000/= kwa mwezi. Nimeshindwa namna ya kujibana ili nimalizie Nyumba yangu.

Msaada wa mawazo jamani..Bado naendelea kuwaomba ushauri Mimi wanajf ndiyo washauri wangu.
 
Kwa mwezi Salio sh60000 tu.Kipato nje ya mshahara sina.Niko maeneo Mapya.Nilijaribu kilimo mazao yamekauka

Kopa kwenye asasi yoyote ya mikopo hako ka ajira kako kawe mdhamini ili uanze kutumikia makato.Kwa kusave huo mshahara mdogo mno.
 
Kwa mwezi Salio sh60000 tu.Kipato nje ya mshahara sina.Niko maeneo Mapya.Nilijaribu kilimo mazao yamekauka

Ungejibu kwa sequence maswali niliyokuuliza ningepata cha kukushauri...ukisema unabakiwa na 60,000 baada ya matumizi yote unaacha loop nyingi! Nataka kujua kama una familia kwa sasa na mkeo anafanya nini sasa, nataka kujua kama umepanga na pango kwa mwezi, nataka kujua matumizi yako yasiyokuwa ya lazima kama unakunywa pombe and likely....kama hutojali unaweza kuainisha pia aina ya kazi unayofanya pia!
 

Kazi Mimi ni MWALIMU mke wangu ni mama WA nyumbani matumizi ni vocha sh25000 umeme sh 18000 Zuku sh19000 maji sh 10000 chakula sh.180000
 

Kazi Mimi ni MWALIMU mke wangu ni mama WA nyumbani matumizi ni vocha sh40000umeme sh 18000 Zuku sh19000 maji sh 10000 chakula sh.258000
 
Kazi Mimi ni MWALIMU mke wangu ni mama WA nyumbani matumizi ni vocha sh40000umeme sh 18000 Zuku sh19000 maji sh 10000 chakula sh.258000

Mwalimu kwanza pole kwa majukumu mazito ya kufuta ujinga kwa vijana wetu....
Kwanza kabisa kwenye kipengele cha vocha unatakiwa kufanya review upya maana matumizi ya 40,000 kwa mwezi kwa simu isiyoingiza fedha si ufujaji tu bali unastahili kujitathmini upya maana si bure michepuko inahusika hapa!

Kwa mwalimu aliye occupied enough na schedule ya kazi sijui huo muda mkubwa namna hiyo wa mawasiliano unaupata wapi...labda ungekuwa hujaoa ningesema unajenga msingi bora kwa proposed mke of whom unaye tayari!

Sitahoji matumizi ya maji wala chakula ila nataka pia uondoe dhana kwamba mkeo ni mke wa nyumbani kwa kumwanzishia kamradiambacho katakuwa kanainua kipato cha familia as well...sina hakika na umbali wa nyumbani kwako na kituo chako cha kazi ila kama navyowaza ndivyo nadhani shemeji akipunguza muda wa kuangalia Zuku angeweza kuandaa chapati,mandazi,kalmati ama kufunga karanga ambazo angekuwa anasambaza kwenye maduka ama ofisi kwa makubaliano maalum ambapo angefanya makusanyo siku ya pili kabla hajaacha mzigo mpya!

Kama hamna matumizi mengine yasiyo yamsingi ni imani yangu kwamba salio utakalokuwa unasave kwa kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili utamalizia nyumba yako na kuingia kitu ambacho kitakuinua kwa kuwa kiwango ulichokuwa unalipa kodi utakifanyia mambo mengine ya maendeleo!
 
Kazi Mimi ni MWALIMU mke wangu ni mama WA nyumbani matumizi ni vocha sh25000 umeme sh 18000 Zuku sh19000 maji sh 10000 chakula sh.180000

Kazi Mimi ni MWALIMU mke wangu ni mama WA nyumbani matumizi ni vocha sh40000 umeme sh 18000 Zuku sh19000 maji sh 10000 chakula sh.258000

Kwa mwezi Salio sh 60000 tu.Kipato nje ya mshahara sina.Niko maeneo Mapya.Nilijaribu kilimo mazao yamekauka

Unnecessary spending..

Na pia andika kama mwalimu.
 

Nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi ingawa Niko kama km 10 toka mji ulipo.
 
Bro, kujenga inawezekana. Na ni kwa sababu hii: Ujenzi huweza kufanyika kwa awamu awamu! Chukulia mfano wa mchwa wanaojenga kichuguu, little by little and after sometime you will achieve an immense feat!

Angalizo, kuna hatua za ujenzi zinahitaji nguvu kubwa: mfano kuezeka! Huwezi kuweka 'roof structure' a.k.a makenchi in place then ukasubiri after sometimes uje uweke 'roof covering' a.k.a mabati

Nakushauri, pata makadirio & nunua material mdogo mdogo tunza, then unakuja malizia na hela ya fundi kazi inafanyika.

Msisitizo: Usitunze fedha, Nunua vifaa vya ujenzi 'building materials' kwakua fedha inapungua thamani kila uchao, fedha ni rahisi kuitumia nje ya mpango. Ila kama una trip ya mchanga, lazima itatumika kama ulivopanga, ni nadra sana kuuza ili fedha uitumie otherwise!

Usidharau 60k, hyo ni trip moja ya mchanga ama mifuko,at least minne, ya saruji. Na mfuko mmoja kitanzania-tanzania unaweza fyatua tofali za inch tano zipatazo 40! Usikate tamaa, you don't have to be paid millions to build a house.

Just stay focussed, determined and you will make it!
 
Hongera sana kaka kwa hatua uliyofikia :yo:,

Mkuu, kabla ya yote tafuta fundi ujenzi akupe tathmini ya vifaa vyote vitakavyohitajika kwa wewe kuezeka. Baada ya hapo nakushauri nunua bati kidogo kidogo weka ndani hadi zitakapotimia kwa kuezeka nyumba nzima. Baada ya hapo tunza hela ya kununua mbao za kenchi na ya fundi pia.

NB: Usithubutu kununua mbao na kuweka ndani huwa zina tabia ya kupinda zikikaa muda mrefu. Mengine wataongezea wengine.
 

Mfawidhi nakushukuru sana.Umenipa matumaini kimsingi kumbe watu bila ushauri ndiyo mana tunaanguka na kufa kwa pressure. AKSANTE SANA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…