Kwa kawaida mauziano ya mali zisizo hamishika ni vizuri yakahusisha mamlaka za eneo husika mfano, mwenyekiti wa mtaa nk, lengo kuu ni kujihakikishia kuwa mali inayouzwa na anayeuza anatambulika, lakini kwa kua hilo halikufanyika maana yakae nikua ardhi hiyo haina security ya kutosha, nashauri kabala ya hatua yoyote pateni mtaalamu wa ramani(land surveyor) ili achukue coordinate za eneo husika kujua serikali imelipanga kwa matumizi gani maana kuna cases nyingi unauziwa eneo halijapimwa baadae unaambiwa nusu nzima imeangukia barabarani, endapo eneo litabainika kuwa Katika mpango sahihi sasa mnaweza kufanya mauziano kwa kushirikisha viongozi wa serikali za mtaa husika, ni kawaida hua wanachaji vi pesa kidogo but kw ajili ya security ni vema ufanye hivyo.