vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 895
- 571
Salamu wana JF. Kuna mtu ameniomba msaada wa ushauri, nimeshindwa kumshauri maana mambo ya sheria sijui. Rafiki yake anataka kumuuzia nyumba iliyojengwa kwenye eneo ambalo bado halijapimwa. Karatasi ya ununuzi wa eneo hilo iliandikwa bila kushirikisha serikali ya kijiji, yaani iliandikwa kienyeji ingawa kulikuwa na mashahidi. Je afanyeje ili aweze kuinunua nyumba hiyo kihalali ili siku za usoni asipate matatizo? Msaada wa kisheria tafadhali.