Msaada: Kuhusu Uraia

Msaada: Kuhusu Uraia

NDESSA

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Posts
1,946
Reaction score
1,796
Habari wakuu,

Naomba kujua kama wazazi wamehamia Tanzania kutoka nchi nyingine na Baba akapata uraia wa kuandikishwa na mama hajapata je mtoto atakayezaliwa Tanzania mzazi mmoja akiwa na uraia ili mtoto huyu awe Raia kamili nini kinatakiwa kufanyika?

Natanguliza shukrani.
 
Hapo mpaka huyo mtoto atakapofikisha umri wa miaka 18 ndio ana uwezo wa kuchagua awe mtanzania au nchi nyingine.
akiamua kua mtanzania atakua amepata CITIZENSHIP BY BIRTH
nawasilisha!
 
Asante sana mkuu kwa maelezo yako, Je kufanya huo mchakato anaenda Mahakamani au kwenye chombo gani?
 
Kama mtoto alizaliwa baada ya baba yake kupewa uraia wa kuandikishwa, automaticaly mtoto anakuwa raia wa Tanzania kwakuwa baba yake ni Mtanzania tayari wala haitiji kwenda mahakamani. Ila akifikisha umri wa miaka 18 anauwezo wa kuamua kufuata uraia wa mama yake, na kwakuwa nchi yetu hairuhusu uraia wa nchi mbili itampasa kuukana uraia wa Tanzania na kupewa huo wa nchi ya mama yake.
 
Asante sana kwa maelezo yako mazuri.
 
Back
Top Bottom