Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa chagamoto hiyo, surveyor kutoka TANESCO halipwi na mteja, kufika kwako kutoa huduma ni majukumu yake ya kazi na analipwa na shirika, usifanye malipo yoyote ili kupata huduma hiyo tafadhali.^OKHabarini wadau? Nimewauliza TANESCO kwenye thread yao hawajanijibu nimekuja kuomba msaada huku. Je, surveyor kutoka TANESCO analipwa na mteja anayehitaji kuunganishiwa umeme ndo aje afanye survey nyumbani kwako au ni bure?? Nimeuliza hivi maana mimi nimeambia nitoe pesa ili mtoa huduma hiyo kunifikia.