vvti engine
Senior Member
- Nov 15, 2018
- 188
- 209
Heshima kwenu Wana jukwaa. Kama mada ilivyo, nilipigiwa simu na kitengo Cha huduma kwa wateja Cha Vodabima, wakidai nimekidhi vigezo vyote vya kujiunga na huduma yao ya Vodacom Bima. Maelezo Ni kuwa kwa idadi ya watoto wangu pamoja na mtegemezi mmoja ninatakiwa kulipia huduma hii TSHS. 7,500/= kwa Kila mwezi.
Nikaambiwa kwa kiasi hicho nitapata AINA tatu za bima. (1) Bima ya ajali (2)Bima ya afya au matibabu na Bima ya Maisha. Walinipa maelezo mengi tu Kuhusu michanganuo ya hizo Bima pamoja na mengine mengi. Ninachoomba kufahamishwa hapa Ni ufanisi wa hizi Bima.
Je, kuna mtu yeyote anaye au aliyewahi kuitumia Bima hii ya Vodacom? Vipi Kuhusu utendaji wake na changamoto? Maana wanasema ukitibiwa unatoa pesa yako halafu wao watakurudishia baada ya kuwatumia vielelezo, je Ni kweli wanafanya hivyo? Naomba kuwasilisha.