Msaada kuhusu wakala wa pesa kwenye mitandao ya simu kulipa presumptive tax

Msaada kuhusu wakala wa pesa kwenye mitandao ya simu kulipa presumptive tax

hmjamii

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
627
Reaction score
312
Salaam kwenu!
Naomba msaada kwa wataalamu wa masuala ya kodi, nimejaribu kutafakari kuhusiana na Mawakala wa mitandao ya simu kulipa kodi ya makadirio (presumptive tax) ya mwaka,

Ninafahamu kuwa Wakala anapopata Commission yake ya mwezi huwa tayari imekatwa kodi na huwa hana namna anaweza kukwepa hiyo kodi ya 10%. Kwa wenye kujua taratibu na kwanini WAKALA anatakiwa kulipia kodi TRA wakati kodi analipa kwenye commission anazopata anisaidie na Mimi niongeze uelewa.

Wasalaam.
 
Kodi inayokatwa kwenye commission ipo katika aina ya kodi iitwayo withholding tax(kodi ya zuio) ambapo anayekulipa iyo commission anazuia 10% ya commission yako, kwa mfano commission yako ni 1000,000 basi 100,000 itakuwa kodi. Anayezuia kodi hiyo huitwa withholding agent ambapo yeye huzuia na kukusanya kisha kuwasilisha TRA

Iyo presumptive tax unazungumzia kitu kingine japo nayo ni income tax(kodi ya kipato). Hiyo ni aina ya kodi ya kipato ambayo hukatwa watu wanaozalisha kipato (siyo makampuni) pia wawe wazawa(resident individuals) ambao mauzo yao kwa mwaka hayafiki million 20.
 
Back
Top Bottom