msaada kujibu mashtaka kwa mwajiri.

msaada kujibu mashtaka kwa mwajiri.

JipuKubwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2013
Posts
2,341
Reaction score
2,390
Ndugu wanjamvi, naomba msaada wa kisheria juu ya mashtaka aliyofunguliwa rafiki yangu na ofisi ya TSD, MASHTAKA ni haya; 1;kuvunja kanuni za utumishi wa umma kwa kusema serikali imeoza.
2;Kumdharau mkuu wa wilaya, kwa sababu hayo maneno yalisemwa kwenye kikao na mwenyekiti alikuwa ni mkuu wa wilaya. Hii na kwa mujibu wa hati ya mashtaka. Naomba kwa mwenye ujuzi atusaidie.
 
Mkuu weka vifungu vilivyovunjwa, km kumdharau DC kwa mujibu wa kifungu kipi, Sheria/Kanuni ipi, nk! Funguka zaidi ili usaidiwe...
 
sawa mkuu, kwa mujibu wa hati ya mashtaka kutoka TSD vifungu vilivyo vunjwa ni;1.kukiuka maadili ya utumishi wa umma kanuni namba 42 kifungu cha 4 jedwali la kwanza sehemu A ya mwaka 2003.Na 2.Kutotii mamlaka kanuni namba 42 kifungu cha 3 jedwali la kwanza sehemu A ya mwaka 2003. Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom