Mie sio mwanasheria ila nashauri kwa muono wangu.
Kwanza Pole sana kwa janga hilo,na ni funzo pia,maana kwa Wakurugenzi wa Ulaya wengi wangeweza,maana hawavamii,ila kwa Bongo hapa kila mmoja mjuaji na kila mmoja kuuza sura kwa dem wake kwamba Mie mkurugenzi fulani bila kuweka juhudi kwenye biashara.
Na Sio siri kwa biashara zetu za kawaida kama wajasiriamali kuwa watu 4,ni tattizo,yaani lazima tu mmoja atazingua kwenye safari.
-Kujitoa kwenye Kampuni bila kudai chochote sio kigezo cha kushawishi kujitoa kwako.
Maana kama kampuni ina madeni basi huwezi kujitoa kirahisi namna hiyo
-Jingine ni Suala la namna mlivyosajili,hili ni suala la kufanya amendment tu kwenye usajili wenu kuanzia mwanzo hadi mwisho.
-Ukurugenzi unaweza kuwa na mfumo wa hisa,sasa unaweza wewe ukauza hisa zako kwa wakurugenzi wenzio waliopo,sasa hapa sijui kama utauzaje,maana inaonekana kwamba itakuwa Zero share.
Ushauri:-
Mfuate mwanasheria wenu alieandaa Memorandum yenu na kushughulikia suala lenu wakati wa kufungua Kampuni.
Sasa kwake huyu ni rahisi saana kukusaidia hili,maana Kampuni zinatofautiana kiuendeshaji,na hii ndio inauwezo wa kujua ni jinsi gani unaweza kujitoa.
Maana pia inatia shaka kwamba,inakuwaje unataka kuondoka kwenye Kampuni bila kudai kitu(Hapa natia hofu kiasi)
Watakuja wadau wengine