Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Asante Mjomba, umeiweka vema sana hii kitu. Hawa watoto hawajawahi kujenga.
Kwenye uimara wa Tofali mbali ya ratio ya mchanga na simenti, pia utaalamu wa Fundi kwenye uchanganyaji una nafasi kubwa pia.
 
Upo wapi mkuu?

Kila mfuko mmoja wa cement toa tofali 45.

Mchanga utahitaji wastani wa lorry 18 za ujazo wa 4.7mm3.

Gharama ya kufyatua mfuko mmoja wa cement ina range 5000-7000

Kwa ushauri zaidi nicheki PM
45! Inabidi cement iwe 42.MPa na mchanga usiwe na mboji, maji yawekwe kwa kiasi kidogo na yasiwe na kemikali kama chumvi na mashine itumike kukandamiza mchanganyiko wa cement maji na mchanga!
Ukitumia 32.5 MPa cement, ukatumia mkono kukandamiza tofali zenyewe nakadhalika! Basi nadhani Utakuwa unampoteza ndugu yetu! Yangu ni hayo!
 
Mkuu, uministua!
 
Kwa hayo maeneo acha kabisa mawazo ya kufatua matofali ya kupiga Kwa mkono,
Kanunue tofali za mashine mpaka 1100 watakuuzia na watakuletea mpaka site na kama utataka kupiga za mkono Kwa mfuko zisizidi total 35!
Asante kunishauri. Nilishaamua sitanunua tofali bali nitakodisha nifyatulie nyumbani lengo likiwa kuokoa gharama kiasi fulani, nadhani kikubwa natakiwa niwe makini ili tofali zitoke imara na hili naona linawezekana kabisa. Lazima nitatumia cement ya 42.5plus
 
Yes lazima nitumie cement ya 42.5
 
Gharama halisi itategemea na mahali ulipo:-
Mahitaji ni kama ifuatavyo
1. Saruji mifuko 107
2. Mchanga lori 15 za tani 3.5 ambapo lori moja itafyatua mifuko 7
3. Gharama ya kufyatua mfuko mmoja wa saruji ni shiling elfu 5 mpaka 7
4. Maji itategemea na mahali ulipo na upatikanaji wa maji eneo hilo.
5. Kwa mifuko hiyo 107 utapata tofali zisizo pungua elfu 5 kwani kuna wakati mafundi watachanganya saruji na kujikuta mfuko umetoa tofali 50,48,45,au 44
Kupata kiasi cha hela kinachohitajika fanya hesabu kwa kupitia hizo figure hapo juu
 
Sawa mkuu

Haya ndio walitaka kumletea Magufuli wakati wa kujenga bwawa la Nyerere. Ulichosema ni kweli tupu hakuna kitu hapo. Water should be clean for what?

Ni kutisha watu tu wakati vitu vinawezekana
Hawa wanaleta habari zao za google Tanzania hii hakuna jengo limejengwa kwa uwiano wa tofali 20 kwa mfuko mmoja wa saruji, hakuna na narudia hakuna. Hizi tofali tunazonunua site zinatokana na uwiano 1:50 mpaka 60.

Habari za serikali hizo data zinatumika kuendesha upigaji. Wachina waliojenga kile chuo cha Siasa pale Kibaha wametumia tofali toka kwa site ya mtu binafsi mbona kimepasishwa
 
1: Mfuko mmoja 42 ..tofali 40 (standard)
2: Mfuko mmoja fundi ni 6,000 (elfu sita)
3: Kwa siku fundi anapiga mifuko 10
4: Mchanga mende ni 220,000-240,000....mende mbili zinapiga tofali hizo na kubaki labda wasijaze vizuri
5: Tofali mchawi maji, power to you
 
Kwani wanaouza tofali wanafavyatua tofari ngapi kwa mfuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…