Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

aina ya mchanga nayo ina tija sana kwenye wingi wa tofali mara nyingi sana ukitaka tofali bora kabisa kwa kanda za mikoa yenye maji chumvi yaana mikoa ya kanda ya kati na pwan pamoja na baadhi yanmikoa ya kanda ya ziwa angalau ukitumia 32.5R kwa mkono basi ili tofali Iwe bora basi anzia tofali 30-35 na kwa cement ya 42.5R basi tofali anzia 36 hadi 45 hizo ni za mkono hapo utapata tofali bora kabisa.

ila kwa ukanda wa nyanda za juu kusini yan mbeya huko na kaskazin ya arusha moshi huko basi cement ya 32.5R angalau tofali 36 hadi 50 na cement ya 42.5R angalau tofali 51 had 65 hapo utapata tofali bora kabisa

NB: Maelezo hayo ninkwa cement ambayo haijazidisha siku 6 hadi 10 tangu itoke kwenye mkanda. kadri inavyo zidi kukaa ndivyo na idadi ya tofali inavyo pungua
 
tofali zinataka vitu muhimu vifuatavyo ili kuliboresha
1. aina ya mchanga hapa zingatia mchanga wenye punje kubwa kubwa usiwe powdered sana
2. mchanganyiko mzuri wenye vipimo sahihi kati ya maji mchanga na cement
3.umwagiliaji maji ya kutosha baada ya tofali kufyatuliwa
ukizingatia hayo tofali litatoka imara kabisa.
 
Nipo mbeya mwezi huu nataka kufyatua tofari, mfyatuaji aliniambia ratio nzuri kwa cement ya 42.5 ni tofari 35,kutokana na huu uzi nitafanya research kidogo, namwambia afyatue tofali 40 kwa mfuko kwa mifuko 10 kwanza, napiga Maji ya kutosha afu nasimamia mwenyewe mwanzo mwisho nione ubora wa hilo tofari ukoje, tutaleta mrejesho humu
 
Upo wapi mkuu?

Kila mfuko mmoja wa cement toa tofali 45.

Mchanga utahitaji wastani wa lorry 18 za ujazo wa 4.7mm3.

Gharama ya kufyatua mfuko mmoja wa cement ina range 5000-7000

Kwa ushauri zaidi nicheki PM
Safi sana mkuu
 
Asante kwa uchambuzi. Kumbe hakuna faida ni usumbufu wa bure
 
Upo wapi mkuu?

Kila mfuko mmoja wa cement toa tofali 45.

Mchanga utahitaji wastani wa lorry 18 za ujazo wa 4.7mm3.

Gharama ya kufyatua mfuko mmoja wa cement ina range 5000-7000

Kwa ushauri zaidi nicheki PM
Aiseee
 
Mchanga unaweka ndoo ndogo ngapi?
 
Mrejesho?
 
Tofali 45 kwa mfuko wa sement ya 42.5 standard ni sawa kabisa tena mafofali imara sana, issue hapo ni mchanga mzuri na kunyeshea maji ya kutosha basi, ubora wa tofali ni curing, mchanga bora na proper mixing basi,
 
Hizo tofali ni za fensi sio nyumba utanishukuru fanya tofali 40 kwa mfuko. Na inategemeana na aina ya mchanga kama una chumvi ama udongo utafanya chini yaa hapo.
Utapiga hesabu mwenyewe
Trip moja ya 4.5qm hufyatua mifuko 7
Kila mfuko hutoa tofali 40
Kufyatua ni 6000 kwa mfuko
Kumwagilia weka laki 1 hadi siku 10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…