Anaweza kuwa amemeza mdudu fulani yuko kama chura (sijui jina lake halisi) mdudu huyu haozi haraka na humsababishia kuku kuwashwa kooni kwa sababu ya sumu yake.
Mara nyingi kuku hukohoa ama kukoroma kama binadamu hasa nyakati za usiku.
Koroga chumvi iwe kali kiasi, mnyweshe. Hii husaidia huyo mdudu kuoza haraka. Fanya hivyo hivyo kila jioni kwa siku tatu.
Waweza pia kufuata ushauri wa kumuona daktari wa mifugo kama ulivyoshauriwa, iwapo kuku wako anaugua mafua ya kawaida.
Habari,jamani naomba msaada wa haraka kuku wangu jogoo wa malawi anaumwa mafua hadi namuonea huruma yamembana kiasi cha kukoroma na kuziba mdomo, sijampatia dawa yeyote naomba mnisaidie aina ya dawa nzuri na bei yake
Naomba mnisaidie maana nimemnunua ili nipate mbegu akifa nitaumia sana
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Habari jamani;
Naomba msaada wa haraka kuku wangu jogoo wa Malawi anaumwa mafua hadi namuonea huruma yamembana kiasi cha kukoroma na kuziba mdomo, sijampatia dawa yeyote naomba mnisaidie aina ya dawa nzuri na bei yake. Naomba mnisaidie maana nimemnunua ili nipate mbegu akifa nitaumia sana.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mafua ya kuku ni hatari. Kama huna hela kwa sasa chukua kidonge cha tetracycline kipasue changanya kwenye maji umnyweshe haraka. kwa vile ni ugonjwa wa kuambukiza unaweza kuwapa kwenye maji na kuku wengine ili wasishambuliwe mpaka hiyo jumapili utapopata hela ya chanjo.