nina wasiwasi ni mafua ndo kuku husinzia ila kwavile hatuwaoni bora uwatafutie dawa ya mafua ambayo ni broad spectrum yaani inatibu na magonjwa mengine mf fluban au OTC kuliko kusubiri jtatu
Kwa bahati nzuri nilicho kuwa natafuta imekipata. Leo asubuhi nimekuta kuku wawili wana umwa mafua nikawatenga alafu kaenda tafuta dawa bahati mbaya leo J/pili maduka yote nimekuta yamefungwa.
Hivyo nikarudi nikawapa Antibiotic ( Vertox 20. spelling nimesahau kidogo) ili kesho nikawanunulie dawa ya mafua.
Mama Joe, sijui itakuwa sahihi kesho kuacha kutumia hiyo antibiotic nikaanza dawa ya mafua?
angalia hali yao hadi asubuhi ikoje kama wana nafuu waweza endelea ukaachana na dawa mpya. Pia jifunze kusoma composition ya dawa unaweza kuwa ni tetracycline ukaenda ukauziwa hiyo iyo kwa trade mark tofauti. Kuliko wajaza madawa endelea nayo ila kama hamna unafuu ukifika waambie wazi umetumia hiyo ili wasijekukupa iyo iyo
Ahsanete sana Ndugu, Nitajitahidi sana kufuatilia Mama Joe.
Mama Joe naomba msaada wako kuhusu uhalali wa matumizi ya dawa aina ya TEMEVAC NDV STRAIN 1-2 kwa ajili ya chanjo. Ni ile ya matone ya kuweka machoni.nina wasiwasi ni mafua ndo kuku husinzia ila kwavile hatuwaoni bora uwatafutie dawa ya mafua ambayo ni broad spectrum yaani inatibu na magonjwa mengine mf fluban au OTC kuliko kusubiri jtatu
Mama Joe naomba msaada wako kuhusu uhalali wa matumizi ya dawa aina ya TEMEVAC NDV STRAIN 1-2 kwa ajili ya chanjo. Ni ile ya matone ya kuweka machoni.
Ndiyo.ni chanjo ya kideri? Mimi sijawahi itumia maana navyosikia sio nzuri kama ya maji
Ndiyo.
Nilifanya consultation kwa mzee mmoja mtaalam wa mifugo, mi nilikuwa natafuta dawa ya chanjo lakini niliyoikuta kwenye maduka mengi ni ile ya kidonge ya kuchanganya na maji. Baada ya kupewa maelekezo yake nikaona mashariti ya namna ya kuihifadhi ni magumu kwa mazingira ya vijijini, hivyo yeye aliniambia uwepo wa hii dawa ya matone na kuwa ilikuwa imeondolewa kwenye mzunguko kwa kuwa ilichakachuliwa hapo awali. Lakini akaniambia kwa sasa imerudishwa na inafanya kazi. Nilifikiri labda unawezakuwa na taarifa kuhusu kurudi kwake ndo maana nilikuuliza.
Nimeichukua leo na kuituma kijijini kuku walipo. Basi ngoja nifanye kama majaribio ingawa sasa kama bado ina madhara kuku wangu wafa jamani!!
ni chanjo ya kideri? Mimi sijawahi itumia maana navyosikia sio nzuri kama ya maji
Hata ya maji nayo ni shida tupu, Wafanya biashara si waaminifu, unaweza kuta umeme ilikatika siku nzima au frdge ikaharibika na Dawa yote kuharibika ila hawawezi sema wanauza hivyo hivyo matokea yake mtu anawapatia kuku na bado wanakufa kwa Kideri
Jaribu kucheki na watu wa wizara kama kweli imeruhusiwa make Wabongo kwa kuchakachua hatujambo, unaweza uziwa iliyo isha muda wake, na Hizo dawa huwa ni za Serikali, na hayo maduka huwa wanauza kwa wizi tu.