Msaada: Kuna aliyekutana na hii "2020 Annual Visitor Survey" kutoka Opera Browser?

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,508
Reaction score
2,619
Habarini,

Mimi ni mtumiaji mzuri wa Opera Browser, yaani huwa sina mtindo wa kupakua Apps kujaza kwenye simu.

Kutokana na hilo leo kila nikijaribu kuingia kwenye internet web yoyote unakuja ujumbe usemao "Dear Opera user, you are today's lucky visitor for April 5 2020. Please complete a short survey and to say THANK YOU we'll give you a chance to get Samsung Galaxy S10.

Nimemaliza hiyo survey baada ya kushindwa kabisa kuperuz kutokana na kuletewa ujumbe huo kila mara.

Kwenye hyo survey, kuna maswali manne na nimejibu yote na nikachaguliwa kupata zawadi. Baada ya hapo ikaja page ya kujaza kama fomu (majina, email na ZIP. Sasa hapo kwenye ZIP ndio mtihani kwangu, NITAPATAJE? Kuna yeyote humu JF kakutana na hii? Maana kwa chini kuna comments za watu wakishukuru kupata (kupokea) zawadi zao. KARIBUNI.
 
Mkuu opera part yake imenunuliwa na wachina, wanachofanya sasa hivi ni kukujazia matangazo, na mambo mengine kama hayo ili wapige hela, pengine hio s10 ipo moja na mliofanya survey ni zaidi ya milioni 10. Opera ya sasa si kama ile ulio izoea.
 
Mwamba287 said:
Apo jaza namba zozote 5 Naskia Tanzania hatuna zipcode
Sawa mkuu. Hivi zipcode na postcode ni vitu viwili tofauti ama?
 
Nilikutana nayo hii nikaona kama wananitania nikaachana nayo! Yaani nipate s10 kwa maswali mepesi halafu ya kuchagua. Nikajaza nikayapatia yoote, nilipoona mambo ya zipcode nikaachana nao nikaona huku mbele tusijeanza kuambiana tuma hela ya kusafirishia, Nikaona hawa ni miyeyusho,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikutana na ya Tigo kwenye chrome ila baada ya kupatia maswali wakaleta mambo ya kujaza information ikabidi niachane nao maana hiyo information huwezi jua wataitumia vipi
 
Thanks kwa ushuhuda mkuu. Vipi kuhusu zipcode kwa hapa DAR?
 
Extra Miles said:
Nilikutana na ya Tigo kwenye chrome ila baada ya kupatia maswali yote wakaleta mambo ya kujaza information nikaachana nao maana huwezi jua hizo information watatumia vipi
Shukuran mkuu.
 
Drone Camera said:
Mzee potezea tu kuhama kutoka kitochi 4G si rahisi kihivyo
Ndo maana nlikuja hapa nipate ushuhuda kwanza. Vipi kuhusu zipcode?
 
Aiseee mwenyewe Zip walihitaji sasa nilichokufanya niliingia google nikaipata kulingana na sehemu niliopo sasa ikatakiwa kujaza account yangu ya visa au Master aiseee nikajaza ambayo haina hela eti wanagoma wanataka yenye hela aiseee hapo ndio ikawa mtihani lakini zip code yenyewe waliikubali.
 
Opera Matapeli sana.

Tena siku hizi wameruhusu watu walipwe wakiandika articles kwenye Opera News basi imekuwa The Home of Fake News and Conspiracy Theories
 
Chief-Mkwawa said:
Kama hakuna postal code baadhi ya form ukiweka postal code wanaikubali tu, otherwise google yoyote weka ila kibongo bongo hatuna zip code
Nimekuelewa CHIEF.
 
Humphrey Mrema said:
Ni kitu kimoja, ZIP code inatumika sana Canada na Postal code inatumika zaidi Marekani
ZIP code ni sawa tu na Postal code, yaani sanduku la posta.
Sawa mkuu kwa hyo sehemu ya kujaza ZIP code una maana kwamba naweza kuweka sanduku la posta la mahali nilipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…