Msaada: Kuna Mume kapigwa na kitu kizito, naomba tuwashauri

Msaada: Kuna Mume kapigwa na kitu kizito, naomba tuwashauri

Victoire I'm assessing suck kind of scenario.

Kuna binti yuko Tanzania, mbali na mimi, nataka nimwambie aendelee na maisha yake na mimi nifanye mpango wa familia mpya, ila bado moyo unakataa..
Mwambie tu,ila akifanya kweli baaae usimlaumu.
 
Iko hivi hawa mke na mme wanaishi nchi tofauti ila hapo nyuma walipendana sana tena sana na.wana watoto kadhaa. Sasa mme akapata michepuko hapa Tanzania.

Na kuna mchepuko aliupenda sana sana kupita mingine. Mke wake anaishi London na watoto. Sasa kuna siku mme akampigia mkewe simu akimwambia kuwa hamtaki tena na huyo mke anaweza endelea na maisha yake.

Mke alichanganyikiwa ila mme alisimamia msimamo wake. Basi ikabidi mke aikubali hiyo situation.

Hapo ilikuwa katikati ya 2020.Mke alihitaji mtoto mwingine hivyo akaamua kwenda kupandikiza mimba ya sperm donner asiyejulikana.

Maisha haya jamani. Kumbuka mme alimuacha huyu mke kwa matusi na udhalilishaji ingawa hawakupeana talaka rasmi.

Bwana we 2022. Mme yakamfika hapa. Akaamua kwenda UK kumuona mke na watoto. Si akakuta mwanamke ana Mimbaaaaa.

Mwanaume alidata. Hapa ndo patamu ilibidi mwanaume ageuze kurudi Dar eti akimlaumu mke why kabeba mimba ya mtu mwingine?

Tuwasaidieje hawa jamani hasa mwanaume. Maana alimuacha mwenzake kwa matusi leo analia jamoooni.

Wana MMU najua mnabusara tuwasaidie hawa jamani kiushauri.
"Nimekuerewa"
 
Hivi ilikuwaje alipokuwa akipiga mimba haiingii ila kupandikiza ikaingia! Shida inakuwa kwa nani haswa?
Itakuwa ana low sperm account. Inabidi abustiwe ili zikaongezewe nguvu maabara.
 
Simple

Mwambieni huyo mwanaume akale alipopeleka mboga

Alipokuwa anatumia sehemu zake za siri kwa starehe zake mbona hakulia? Alipokuwa anamtukana mkewe mbona hakulia????

Kaachwa/kachunwa mpaka mifupa ndio anajua ana mke


Halafu unajiamuliaje tu kumrudia mtu uliyemwacha kwa matusi kejeli na dharau?

Alidhani mke hana sehemu za siri anazo yeye tu????

Akubaliane na hali halisi, asepe moja kwa moja kama alivyodhamiria mwanzo, au kama mkewe atamkubali basi amkubali mtoto

Mwisho kama huna uhakika na maamuzi yako chepuka kimya kimya bila kumshtua mwenzio
 
Mke kasema kapandikiza hiyo mimba kwa kutumia sperms za unkown sperm donner. Shida hapa mme anamlaumu mke eti kamchanganyia damu. Kumbuka huyu mme alimuacha huyu mama kwa matusi. Ingawa hakukuwa na talaka rasmi.
Na yeye si akachanganye damu?????


Hata kama ameipata hiyo mimba kwa ngono shida iko wapi?????
 
Back
Top Bottom