...mkuu "mathematics" ukifatilia hizo link zina maelezo tofauti' most zikiwa za wadau/wanajamvi wa hapa JF' mimi nikiwa mmojawapo, lakini maelezo yake ya hapa JF hayatoshi kwa mtu mwenye nia yakutaka kununua SUZUKI JIMNY, "mimi nimekuwa nikifatilia aina ya gari kwa muda mrefu, baadaya kuwa nimetumia aina tafauti ya magari, na sasa natafuta gari ya kukaa nalo angalau zaidi ya miaka 10 na zaidi".
Kwavile' ndg yetu
Zanzibar-ASP kaomba kuwekewa link ambazo zote mimi binafsi nimezipitia, na kwa maelezo yaliyomo hayatoshelezi kwa mwenye nia ya kununua gari hilo!
Ndiyo maana nikaweka na LINK za mitandao tofauti za uuzaji wa magari, na ukifatilia kwa udani zaidi utaweza kugundua kasoro/ujanja wanao tumia baadhi ya mitandao (kwa mfano kwenye UBAO WA MATANGAZO WA
TRADECARVIEW kuna makampuni mengi wanatumia mbinu mbalimbali ili kuwapata wanunuzi).
Pia kuna makampuni mengine wako makini kwa uuzaji magari yenye ubora. Kwahiyo mkuu ndugu yetu "Zanzibar-ASP" kama unahitaji kununua SUZUKI JIMNY (ni gari nzuri sana, linahimili misukosuko ya barabarani, matumizi madogo ya mafuta, kwa ujumla ni gari imara, ndiyo maana na bei zake ziko juu):
Ziko aina tatu za SUZUKI JIMNY' zenye cc 0.650 & cc 0.660 ndiyo ze bei ya juu.
"mkuu 'Zanzibar-ASP' fanya utafiti wa kina kwanza"