Msaada: Kuotesha nywele kichwani

Kwahiyo mkuu nywele zilianza kudondoka mojamoja hadi ukajikuta upara huo au ilikuaje?
Nilichogundua kwenye kuoga lile povu kichwani na unaposugua kichwa kinaondoka na nywele dhaifu
 
Mkuu tafuta hela maana ukiwa na hela hakuna bint atakuona na kipara yaani utaonekana na bonge la afro😄😄
 
Kipindi chote nilikuwa nakosaga kujiamini nikijihisi kwamba nina kisogo kirefu sana hivyo nikawa nashindia Cap hivi ninavyoongea majuzi ndo nimegundua kwamba sina kisogo kirefu wala ndo nikaanza ku-enjoy na kichwa wazi
 
Pengine jaribu mafuta ya kitunguu swaumu unapaka yakiwa na mchanganyiko wa asali mbichi , unaacha Dak 30 Kila siku asubuhi jion hrf unasafisha Kwa maji vugu! Pia kipara sio kilema Mzee wangu
 
Ukiambiwa mimi ndio yule jamaa aliyekuwa anafuga rasta zake smart kabisa hutaamini
Shida ilikuja nilipoamua kuzinyoa 2010.
kuanzia hapo ndio niligundua kumbe nilifanya makosa maana nywele zilipoota mzigo ukaanza kuonekana kwa mbali.
Sasa hivi ni mwendo wa dongo tu kila baada ya siku5.
 
KI UJUMLA KIPARA SI KITU NINAPENDA ITOSHE KUSEMA HVYO , HATA KAMA NITAPATA ELA LAZIMA NIRUDISHE NYWELE TUU NI SWALA LA MUDA

NASHUKURU KWA COMMENTS ZETU
 
Hela inaleta kujiamini.
Hela inafanya kipara haionekani.
Hela inaongea yenyewe kwa kila mrembo atakae iona.
Ebu tafuta hela kijana, achana na mambo meeeeengi.
 
Cha msingi jizoeshe kunyoa kipara baada ya muda utazoea tu, utatumia gharama kubwa kuotesha nywele ila matokeo hayatakuwa mazuri.
KIPARA ni desturi tangu 2016
 
Mi nna kipara , lakini n mbishi kwani saloon ninaenda baada ya siku 32....angalia msidhuru afya zenu kwa kutaka kwenda tofauti na vile mwili wenu unavotaka

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
dawa ya kipara ni para mzee
nna Wahl yangu hapa safi kabisa
 
Kwanza kuna aina 3 za vipara
Kipara cha hela
Kipara cha uchawi
Kipara cha elimu
Sjui chako kipo kundi gani lkn dawa yake
Tafuta mafuta ya nyonyo ya kienyeji na mafuta ya sulphur yanapatikana kwenye maduka ya vipodozi
Changanya hayo mafuta uwe unapakaa kichwa kizima ndani ya miezi 3...4 utakaa sawa
 
tumia kitunguu maji tangawiz na kitunguu swaum changany pamoja alaf paka yale maji yake kweny upara wacha kwa dakika 30min to 1hr alaf osha
inaondoa muasho kichwan na mabadiliko utaanza kuonan 1 to 2 weeks
N:B
fanya ivo mara moja per day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…