Mjomba Fujo
JF-Expert Member
- Oct 27, 2012
- 2,438
- 6,313
Wakuu habari,
Nina shida ya kupata bidhaa kutoka kenya, utaratibu upo vipi kusafirisha, kuna material nimezi spot kenya nahitaji kuzileta bongo, nimewasiliana na muuzaji tayari, sasa nahitaji kufahamu ni njia ipi nzuri nitumie ili niweze kuzipata.
NB:
Wale wa Tz vs ke naomba mkae kando.
Nilitaka kumueleza afafanue zaidi kuhusu bidhaa anazotaka kusafirisha ila nikakumbuka hii ni Jf na hata mimi mwenyewe huwa sipendi kabisa kuanika shughuli zangu hadharani. Akianza shughuli yenyewe kama nilivomueleza hapo juu nadhani atafanikiwa bila stress nyingi.Inalingana na kile unachotaka kununua. Hata hivyo, ungefwata kile ambacho pingli-nywee amenena
Wewe sio TZ vs KE?Mkuu wasiliana na mkenya ambaye unanua bidhaa kutoka kwake ili ujue jinsi anavotaka kupokea hela zake. Ukifanya biashara yote hii kupitia benki kila kitu kitakuwa rahisi. Benki itakupa fomu muhimu ya Import Declaration ambayo humo ndani inaashiria aina ya bidhaa, malipo ambayo unatakiwa ulipie bidhaa zenyewe n.k, n.k. Equity huwa wako very fast na ukianza process yenyewe leo hii ikifika jioni watakuwa wametuma fomu yenyewe Dar kwa TISCAN, kampuni ya inspectors ya kitanzania ya kushughulikia imports za aina hizi. Ukisha wasiliana na TISCAN uanze shughuli ya kuzisafirisha kutoka Kenya. Upande wa Kenya hutapata stress nyingi. Utapata usaidizi wote na fomu zote sehemu moja, Huduma Centre iwe boda pale Sirare, Namanga au Nairobi na watakushauri kuhusu malipo yeyote ya ziada.
Ikifika wakati wa kusaidiana kwa hali na mali mbona tusisaidiane?. Hayo mengine huwa matani tuu, wewe unadhania tukipatana na wewe hapa Kenya ama popote pale hatuwezi saidia juu ya ushindani wa JF?. la hasha .Wewe sio TZ vs KE?
Sio kusaidiana, kuna mtu anapigania doo ya saro utafikiri yupo kwenye third world warIkifika wakati wa kusaidiana kwa hali na mali mbona tusisaidiane?. Hayo mengine huwa matani tuu, wewe unadhania tukipatana na wewe hapa Kenya ama popote pale hatuwezi saidia juu ya ushindani wa JF?. la hasha .
Hahaa! [emoji1] Sidhani, kozi ya Tz vs. Kenya niliikamilisha kitambo sana. Utotoni enzi zile nikisoma na watz, tulikuwa tunabishana kuhusu rangi za bendera zetu na wimbo wa taifa na kwa miaka mingi wenzako walikuwa wanapenda kumsifia bondia wao.(alikuwa anaitwa Matumla au?) Alafu tukiwazidia na stori za wachuna ngozi, ambazo zilikuwa zimevuma enzi hizo, walikuwa wanaanza kuimba wimbo flani hivi. "Taaanzaniiia Tanzaniiiaa nakupenda kwa moyo woteee, nchi yangu Tanzaniiiaa jina lako litamu sana weee!...niamkapo asubuhi nakuwaza eweee wanguuu" [emoji23][emoji23]. Utoto raha sana maanake hakukuwa na chuki za aina yeyote ile. Sasa hivi mimi ni mtu na akili zake na hizi ligi za Jf huwa nazichukulia kama utani tu. Isipokuwa hapa kuna wale ambao wamejawa na chuki kweli kweli.Wewe sio TZ vs KE?
Mtoa mada amesema waziwazi, hataki tz vs ke hapa. Sasa nashanga mjomba pingli- nywee kawahi kiti cha mbele.Ikifika wakati wa kusaidiana kwa hali na mali mbona tusisaidiane?. Hayo mengine huwa matani tuu, wewe unadhania tukipatana na wewe hapa Kenya ama popote pale hatuwezi saidia juu ya ushindani wa JF?. la hasha .
Acha zako wewe, mbona watu wa ligi za 24/7 tunawajua vizuri? Kama mimi sifai, basi pia wewe ndio captain na ingefaa upigwe ban ya maisha kwenye uzi huu.Mtoa mada amesema waziwazi, hataki tz vs ke hapa. Sasa nashanga mjomba pingli- nywee kawahi kiti cha mbele.
Mimi napata tabu sana kuamini eti wewe umeacha ligi ya tz vs ke. Nikipitia post zako chache tu nyuma nona bado zina rangi ya tz vs ke. [emoji23]Hahaa! [emoji1] Sidhani, kozi ya Tz vs. Kenya niliikamilisha kitambo sana. Utotoni enzi zile nikisoma na watz, tulikuwa tunabishana kuhusu rangi za bendera zetu na wimbo wa taifa na kwa miaka mingi wenzako walikuwa wanapenda kumsifia bondia wao.(alikuwa anaitwa Matumla au?) Alafu tukiwazidia na stori za wachuna ngozi, ambazo zilikuwa zimevuma enzi hizo, walikuwa wanaanza kuimba wimbo flani hivi. "Taaanzaniiia Tanzaniiiaa nakupenda kwa moyo woteee, nchi yangu Tanzaniiiaa jina lako litamu sana weee!...niamkapo asubuhi nakuwaza eweee wanguuu" [emoji23][emoji23]. Utoto raha sana maanake hakukuwa na chuki za aina yeyote ile. Sasa hivi mimi ni mtu na akili zake na hizi ligi za Jf huwa nazichukulia kama utani tu. Isipokuwa hapa kuna wale ambao wamejawa na chuki kweli kweli.
Haha, ukitaka nipigwe ban peleka maombi kwa JF ukiambatanisha na vielelezo. Tena utakuwa umenisaidia sana kupata muda wa kufanya mengine maana hii JF inakula sana bundle yangu na muda pia.Acha zako wewe, mbona watu wa ligi za 24/7 tunawajua vizuri? Kama mimi sifai, basi pia wewe ndio captain na ingefaa upigwe ban kwenye uzi huu.
Duh! ππππ³Wazee wa ligi ,tz vs kny tunavokatazama haka ka uzi! Tunasubiria hapa pembeni tu[emoji16] [emoji109]
[emoji91] wanasemaga kadamshee...singida- dodoma, mtwara na kigoma-ma-ma[emoji443] [emoji442] [emoji444]
View attachment 874199
πππ JF ni kama mlevi na pombe aina ya pingu, kabla hujaanza kunywa unafungwa kwanza kamba kwenye suruali miguuni maana ukilewa kinachofuata uharo... Kuna muda huwa naamua nisiweke bando lakini kila nikikumbuka mijadala ya humu uzalendo unanishinda...Haha, ukitaka nipigwe ban peleka maombi kwa JF ukiambatanisha na vielelezo. Tena utakuwa umenisaidia sana kupata muda wa kufanya mengine maana hii JF inakula sana bundle yangu na muda pia.
Hao wazee wa TZ VS KE wanataka wakutoe kwenye mada...Acha zako wewe, mbona watu wa ligi za 24/7 tunawajua vizuri? Kama mimi sifai, basi pia wewe ndio captain na ingefaa upigwe ban ya maisha kwenye uzi huu.
Dah! Leo umeniamulia sio bure. Hivi unatarajia mzalendo kama mimi nikalie fence kila mara ndio waniite tikiti maji kama Kalonzo Musyoka? Wakati mnaishambulia nchi yangu? Mijadala ya kutupiana vijembe huwa ina utamu wake wa kipekee ila chuki sina kabisa ndugu yangu. Alafu ukiendelea na hii offensive yako dhidi yangu ntaongea na mawakili wangu jombaa. [emoji1]Mimi napata tabu sana kuamini eti wewe umeacha ligi ya tz vs ke. Nikipitia post zako chache tu nyuma nona bado zina rangi ya tz vs ke. [emoji23]
Aaaah! Nimekuelewa, waambie hawatoniweza, kama hawajipendi wajaribu nimevalia hirizi za Tanga kama hamsini hivi! [emoji38]Hao wazee wa TZ VS KE wanataka wakutoe kwenye mada...
πππ kama hivi?Aaaah! Nimekuelewa, waambie hawatoniweza, kama hawajipendi wajaribu nimevalia hirizi za Tanga kama hamsini hivi! [emoji38]