Mkuu wasiliana na mkenya ambaye unanua bidhaa kutoka kwake ili ujue jinsi anavotaka kupokea hela zake. Ukifanya biashara yote hii kupitia benki kila kitu kitakuwa rahisi. Benki itakupa fomu muhimu ya Import Declaration ambayo humo ndani inaashiria aina ya bidhaa, malipo ambayo unatakiwa ulipie bidhaa zenyewe n.k, n.k. Equity huwa wako very fast na ukianza process yenyewe leo hii ikifika jioni watakuwa wametuma fomu yenyewe Dar kwa TISCAN, kampuni ya inspectors ya kitanzania ya kushughulikia imports za aina hizi. Ukisha wasiliana na TISCAN uanze shughuli ya kuzisafirisha kutoka Kenya. Upande wa Kenya hutapata stress nyingi. Utapata usaidizi wote na fomu zote sehemu moja, Huduma Centre iwe boda pale Sirare, Namanga au Nairobi na watakushauri kuhusu malipo yeyote ya ziada.