Msaada: Kusafirisha vitu toka U.s.a

Jamani posta USA watasafirisha mzigo ukifika Tanzania utaibiwa. Tafuta usafiri wa kuaminika hata kama utaingia gharama kidogo.
 
Hakuna cha kuibiwa utafika vizuri bila tatizo lolote naitumia hii njia sana..lazima waufungue ili watoze kodi ata ukitumia bandari au airport tra lazima waufungue wathaminishe na kutoza kodi...nimetumia njia hii zaidi ya miaka 8...lazima ufunguliwe...mtumaji lazima ajazefomu na aandike kuna vitu gani na mpokeaji jua umetumiwa nini hakuna ujanjaujanja hapo..kila kitu kipo wazi utaibiwa kivipi???
 

Sabasaba una bahati tuu,practically mimi nilituma vitu kutoka US viliibiwa karibu nusu na mbaya zaidi hawatumii hata formula ya kutoza kodi ingawaje naamini ipo wao kazi yao ni rushwa tuu ,sina hamu kabisa na hawa watu wa posta lakini acha waendelee na upuuzi wao maana shirika likifa wao ndio watapoteza kazi
 
Mm nilitumiwa computer mwaka jana kutoka Sweden,nili ipata na sikulipia ushuru,wali niachia kwaku ilikuwa moja,nililipa tu posta fees ilikuwa km elfu 9.
 
thanx mkuu hata mimi nilikuwa natafuta wa kunichukilia mizigo yangu usa. DHL ni expensive sana just imagine unanunua shockups za nissani Maxima kwa dola 200 then uje utume kwa dola mia tiza that is not fair at all. na mimi ninaomba number ya simu ya mr. haji
 
Koba ni kweli kuwa utaratibu wa kutoza kodi haueleweki lakini hii si posta tu ata bandarini na airport utaratibu wa kodi haueleweki kabisa...kuna siku bandarini kodi ya tra bandarini walitaka 6.4ml baada ya kuipinga nikalipa 2.7ml..ata posta kuna siku nilituma flat screen 2 kodi wakataka laki 1.7 lakini baadaye nikalipa elfu 90 ...ila kuhusu usalama sijawahi poteza kitu ni mwaka wa nane naitumia na almost every month natuma kitu
 
Jamani posta USA watasafirisha mzigo ukifika Tanzania utaibiwa. Tafuta usafiri wa kuaminika hata kama utaingia gharama kidogo.

USA ukitumia Express mail, siku 3-4 unaupata mzigo wako.
Ukitumia priority mail, kuanzia siku 10 - 28 utaupata mzigo wako. hapa ndio harufu ya kupoteza mzigo huja.
 
USA ukitumia Express mail, siku 3-4 unaupata mzigo wako.
Ukitumia priority mail, kuanzia siku 10 - 28 utaupata mzigo wako. hapa ndio harufu ya kupoteza mzigo huja.

Vipi kama utatumia priority mail na mzigo ukawa insured?bado kuna harufu ya kupotea kweli mkuu?
 



Wakuu vipi hamjawahi kutuma vitu kutokea UK hivi karibuni??Njia gani rahisi ambayo inafaa??maana kuna jamaa yupo huko anataka kutuma simu so shirika gani ambalo linaweza kusaidia na mzigo ukafika bila kuibiwa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…