Msaada: Kushindwa kumeza Chakula

Msaada: Kushindwa kumeza Chakula

king kan

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
1,639
Reaction score
2,066
Wadau habari za jamvini,

Ninaombeni msaada wenu kwani kila nikila chakula nashindwa kukimeza nahisi kama kinataka kurudi (kama nitatapika).

Tatizo limeanza juzi na linanipa shida kwani siwezi kula lunch au dinner kwa raha, mpaka nilazimishe kumeza tena kwa kutumia vinywaji ili chakula kisirudi mdomoni.

Kunywa vinywaji nakunywa kawaida ila wakati mwingine hata kumeza mate ni shughuli.

Na pia siumwi tonsils na wala sijisikii dalili ya ugonjwa wowote.

Please naombeni msaada wakuu.
 
Sina maumivu yoyote wala sio kichefuchefu inakuwa kama kuna kitu kinazuia chakula kupita mpaka nilizimishe kumeza ila wakati mwingine kinapita kama zamani
Damalu
 
Wadau habari za jamvini,

Ninaombeni msaada wenu kwani kila nikila chakula nashindwa kukimeza nahisi kama kinataka kurudi (kama nitatapika).

Tatizo limeanza juzi na linanipa shida kwani siwezi kula lunch au dinner kwa raha, mpaka nilazimishe kumeza tena kwa kutumia vinywaji ili chakula kisirudi mdomoni.

Kunywa vinywaji nakunywa kawaida ila wakati mwingine hata kumeza mate ni shughuli.

Na pia siumwi tonsils na wala sijisikii dalili ya ugonjwa wowote.

Please naombeni msaada wakuu.

tatizo la kushindwa kumeza linaweza kuwa ni kawaida kama linatokea mara moja na kuondoka ila kama linatokea kwa regural time basi inaweza kuwa ni ishara ya tatizo kubwa, kitaalamu hali ya kushindwa kumeza chakula inaitwa dysphagia na husababishwa na mambo mengi ikiwemo matatizo ya mfumo wa chakula na mfumo wa fahamu.

katika mfumo wa chakula sehemu inayapitisha chakula kwenda kwenye tumbo inaitwa esophagus inaweza kupata matatizo mbambali kama maambukizi ya bacteria,makovu, kutopokea taarifa kutoka kwenye ubongo inayoruhusu chakula kupita,matatizo ya kurithi ,na mengineyo.

baadhi ya mambo yanayoweza kupelekea hali hizi ni:
unywaji wa pombe kali
kuvuta sigara
mdomo kuwa mkavu mara kwa mara
watu wenye ulcers ya tumbo
watu wenye kiungulia
allegy kwa baadhi ya vyakula au vitu kwenye hewa unayovuta
watu waliougua polio utotoni ( post-polio syndrome)

Hali ikizidi pata consultation kutoka kwa madaktari bingwa wa medical surgery.
 
Aksante mkuu reac ngoja niangalie trends na mabadiliko ya hali
 
Mada imenisthtua kidogo, hili tatizo linanisumbua na mimi siku 2 sasa, wacha nimuone Dr. Kumbe huenda ni tatizo kubwa hivyo.
 
Mkuu Smart911 sijawahi hata kuonja hilo unalofikiria na sijawahi kufikitia kufanya hivyo.

Na pia ni vema kuomba radhi kwa kutoa shutuma za kidharirishaji.
 
Mkuu Smart911 sijawahi hata kuonja hilo unalofikiria na sijawahi kufikitia kufanya hivyo.

Na pia ni vema kuomba radhi kwa kutoa shutuma za kidharirishaji.
Elewa kiswahili changu hapo... nimeongea kwa ujumla... kwa maana ya kwamba nimetupa jiwe gizani..
 
M
Elewa kiswahili changu hapo... nimeongea kwa ujumla... kwa maana ya kwamba nimetupa jiwe gizani..
Mkuu angalia context ya quote yako. Pia kama unaona ipo sawa nikutakie baraka za Mungu siku ya leo. Jumapili njema.
 
Kama alivyosema "Reac", hili tatizo ni lazima lichunguzwe kitaalam ili kama niswala la mara moja litibiwe, na kama ni kitu kikubwa kitatuliwe kwa utaratibu wa kueleweka na haraka. Usijaribu kulitatua kienyeji maana unaweza ukachelewa na kuja kujuta baadaye.
 
Back
Top Bottom