Msaada kwa anaejua mambo ya magari Tafadhali

Nkingwamh

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2018
Posts
290
Reaction score
210
Kama kichwa kinavyosema.gari yangu ni Suzuki escudo tatizo kubwa la gari yangu ni shoti za Mara kwa Mara upande wa Betri kwenye positive teminol hadi inafikia muda inatoa moto kabisa nakama nitachelewa kufungua boneti basi gari inaweza kuteketea nimebadiri mafundi ili kumaliza tatizo hilo lakini wapi na hasa ninapotembea safari ndefu ndio hali hii hutokea sasa sijui tatizo ni nini naombeni msaada wakuu kwa anaejua ili nijue tatizo nini ili nikifika kwa mafundi niweze eleza tatizo lenyewe kwani huwa pengine hua wanashuurikia tatizo ambalo sio
 
Tafuta fundi wa uhakika, atafute tatizo lilipo kwa maana haiwezi kuwa ni loose connection kwenye terminal kwa maana angeshaiona. Acheki circuit zote kuona kama kuna excessive drawn of current than rated....na ikibidi acheki wiring yoote ambayo ni kazi ya siku moja tu kwa maana ya saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni!
 
Upo wapi. Hilo nitatizo dogo sana ila nihatari sana. Gari yako inashoti. Tafuta fundi mzuri nasema upo mkoa gani tukupe namba za mafundi wazuri.
 
Mkuu yaani mpaka nachanganikiwa maana huwa wanacheki gari naiacha hadi siku mbili au hata tatu na nikiitwa kuchua naichukua ikiwa safi lakini nikishasafiri safari ndefutu kama kilometa hamsini na zaidi hali hiyo inajirudia
 
Upo wapi. Hilo nitatizo dogo sana ila nihatari sana. Gari yako inashoti. Tafuta fundi mzuri nasema upo mkoa gani tukupe namba za mafundi wazuri.
Mkuu Niko tabora
 
Tafuta fundi wa uhakika, atafute tatizo lilipo kwa maana haiwezi kuwa ni loose connection kwenye terminal kwa maana angeshaiona. Acheki circuit zote kuona kama kuna excessive drawn of current than rated....na ikibidi acheki wiring yoote ambayo ni kazi ya siku moja tu kwa maana ya saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni!
Na kwakuongezeatu ni kwamba kuna wakati nilibadiri Betri yaani ile Betri iliokuja na gari ilikua N40 ya maji sasa Mimi huwa napenda mziki mzuri kwenye gari nikanunua booster wakanifungia mafundi sasa shida ikawa Betri inawahi kupoa nikipakitu kama Massa mwili nikiwa gari nimeizima na swichi ya booster nazima lakini nikija kuwasha haipigi sterter nikanunua Betri mpya ya maji N40 nayo ikawa hivyo ndio mafundi wakanishauri nifunge N50 nilipofunga hiyo ndio tatizo hilo likaanza nikiwa safari ndefu pale kwenye dash board inanipa ujumbe unaosema cheek ijini baada ya hapo nikipuuziatu ujumbe huo naanza kuona moshi upande wa kushoto lililoko betri
 
Ni kama booster imeungwa kutumia umeme wa betri moja kwa moja na haijapitishwa kwenye FUSE, uwezo wa booster ni watts ngapi? Ikibidi weka betri nyingine kwaajili ya hiyo booster yako.
 
Mimi siyajui magari lakini hiyo siyo dalili ya kwamba unatakiwa usilitumie hilo gari mpaka litakapokua sawa? Maana gari kuwaka moto huku upo ndani ni ishara mbaya mkuu.

Anyway ni mawazo yangu tu.
 
Nikweli mkuu kwa sasa nimeipaki nikama siku tatu hivi sijui la kufanya nikaona walau niombe msaada humu
 
Back
Top Bottom