Msaada kwa hili.

Msaada kwa hili.

Lyandembela1

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
277
Reaction score
113
Heshima mbele wadau,

Nimepiga X-ray jana hapa Shree Hindu Mandal Hospital. Moja ya kipimo wanasema moyo umetanuka kidogo. Na daktari kashauri nipime kipimo kinachoitwa ECHO and EGC kwa uchunguzi zaidi.

1: Naomba kujua ECHO and EGC ni kipimo cha nini?

2: Nini kinasababisha moyo kutanuka?

3: Na moyo kutanuka kuna madhara kwa afya, kama ndivyo nini madhara yake?
watu8 MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Kwanini usimuulize Daktari anayekutibu, unaulizia huku?!!
 
Haa haa Miki kaa hauna jibu jibu unapita tuu. Hata utapata ufafanuzi zaidi, na ww pia utajifunza jambo jipya. Sio kucoment tuu.
 
Last edited by a moderator:
Heshima mbele wadau,

Nimepiga X-ray jana hapa Shree Hindu Mandal Hospital. Moja ya kipimo wanasema moyo umetanuka kidogo. Na daktari kashauri nipime kipimo kinachoitwa ECHO and EGC kwa uchunguzi zaidi.

1: Naomba kujua ECHO and EGC ni kipimo cha nini?

2: Nini kinasababisha moyo kutanuka?

3: Na moyo kutanuka kuna madhara kwa afya, kama ndivyo nini madhara yake?
watu8 MziziMkavu


Nitajitahidi kukujibu ikiwa ni kuwasaidia wengine wanaoweza kuwa na matatizo yako. Jibu zuri sana utalipata kwa dakatari wako ambaye ana vipimo vya uhakika kuhusu mwili wako.

(1) Echocardiogram (au Echo) ni kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti yenye frequency ya juu sana (Ultrasonic frequency- zaidi ya mwibi elfu 40 kwa sekunde - 40kHz) kwenda mwilini, halafu kinarekodi mwangwi (echo) wa mawimbi yaliyorudishwa nyuma (reflected) baada ya kupiga kwenye misuli ya moyo. Mwangwi huo huunganishwa na kutengeneza picha ya moyo bila kuharibu misuli ya moyo kama ambavyo x-ray inavyoweza kufanya, kwa hiyo ni kipimo salama kuliko x-ray.

(2) Inawezekana umechanganya Echocardiogram na electrocradiogram ambayo ndiyo hufupishwa kama ECG; electrocardiogram hupima jinsi moyo unavyofanya kazi kwa kurekodi signal za umeme zinazotengezewa na mwili wakati wa mapigo ya moyo, hicho hutoa graphs zinazoonyesha level ya signals hizo kulingana na mapigo ya moyo.

(3) Vipimo vyote viwilli hutumiwa na madaktari wa tiba katika kupima afya wa moyo wa mtu. Moyo kutanuka hutokana na kuwa na high blood pressure kwa muda mrefu sana. Iwapo wewe ni mnene sana, una kisurikari, hufanyi mazoezi yoyote ya nguvu (kama kutembea kwa mguu umbali wa kilometa kama moja au mbili hivi kwa siku), unatumia muda mwingi ukiwa umekaa, unakunywa sana pombe zenye carbohydates nyingi -bia, mapuya, wanzuki, uraka, komoni na pombe za aina hiyo, na vile vile unakula sana vyakula vyenye mafuta ya wanyama kwa wingi ni wazi kuwa unaweza kupata high blood pressure. Kwa bahati mbaya, high blood pressure siyo ugonjwa kwa hiyo mara nyingi huwezi kujua kuwa una tatizo hilo hadi linapokuwa limekuwa kubwa sana na kuanza kuathiri maisha yako. Ni vizuri uwe unapima blood pressure yako mara kwa mara na kulingana na umri wako uhakikishe kuwa haizidi 140/90, ingawa kipimo kizuri kwa watu wote wenye umri chini ya miaka 45 ni 120/80. Kuna vifaa vya kupima blood pressure unavyoweza kutumia nyumbani kwako bila hata kumwona dakatri, kwa mfano hiki hapa chini ambacho bei yake ni kama $50 tu.

hem712clc-1-lg.jpg


(4) Madhara ya moyo kupanuka ni kifo cha mapema. Upanukaji wa moyo huweza kusababisha ugonjwa wa moyo ujulikanao kama Congestive Heart Failure (CHF). Ugonjwa huu husababisha moyo kupungukiwa nguvu ya kusukuma damu mwilini na kukufanya uwe mchovu mara kwa mara. Iwapo itafikia moyo hauwezi kusukuma damu ya kutosha kwenye ubongo basi unaanguka ghafla na kufa hapo hapo. Ubongo hauhimiri hata sekunde moja ya kutokuwa na damu ya kutosha; nadhani umewahi kusikia vifo vingi vya watu kuanguka ghafla na kufa bila kutegemewa. Wengi wao huwa wana matatizo ya moyo pengine bila wao wenyewe kufahamu. Kuna hisisa kuwa PDidy wa Mai aliyeanguka ghafla kule mjini na kufariki huenda alikuwa na tatizo la namna hiyo ingawa hatukupata taarifa za kitabibu.

(5) Kwa bahati mbaya matatizo mengi ya moyo hayaonyeshi maumivu yoyote, ni tofauti na magonjwa kama maralia ambayo unasikia maumivu. Mtu mwenye matatizo ya moyo huwa anaendelea na maisha bila kujitambua hadi pale anapoanguka ghafla na kufariki. Cha kufanya, hakikisha unapima blood pressure yako mara kwa mara na unai control kwa kujizuia lifestyle ya aina niliyotaja hapo juu. Kama una high blood pressure tumia madawa kama daktari atakavyokushauri. Blood thinners, Calcium blockers na madawa mengine utakayoshauriwa na dakari ni lazima uzingatie masharti yake. Ikiwezekana, jenga tabia ya kula vidonge viwili vya asprini kila siku kwani asprini inajulikana kuwa ni blood thinner inayoweza kusaidia kukupunguzia blood pressure.

Mimi siyo tabibu kwa hiyo chambua maneno yangu kwa kutumia akili yako, usiyachukuwe kama ndilo jibu kwa tatizo lako. Onana na daktari wako uongee naye kuhusu afya yako. Jibu langu linatokana na ujuzi wangu wa matatizo ya moyo kutokana na utafiti ninaoufanya sasa hivi katika kujenga teknolojia ya kuwasaidia watu wawezea kujua hali za afya zao mapema bila hata kuonana na tabibu. Nina matabibu kadhaa kwenye project yangu na mimi pia nimesoama sana kujua mambo ya utabibu ili kuweza kukabiliana na changamoto za utafiti huo.
 
Last edited by a moderator:
Heshima mbele wadau,

Nimepiga X-ray jana hapa Shree Hindu Mandal Hospital. Moja ya kipimo wanasema moyo umetanuka kidogo. Na daktari kashauri nipime kipimo kinachoitwa ECHO and EGC kwa uchunguzi zaidi.

1: Naomba kujua ECHO and EGC ni kipimo cha nini?

2: Nini kinasababisha moyo kutanuka?

3: Na moyo kutanuka kuna madhara kwa afya, kama ndivyo nini madhara yake?
watu8 MziziMkavu
kipimo cha Echo kinatazama moyo wote ndani na nje ya moyo na EGC kinapima mapigo yani frequency za moyo wako na zina print.
 
Last edited by a moderator:
NNC umesomeka sana na Miki atakuwa kapata somo pia coz jana alinipalula kwelikweli.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom