Msaada kwa mjamzito wa haraka

matwin

Senior Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
124
Reaction score
134
Habari zenu ndugu zangu.... nahitaji msaada wenu saana. Dada angu ni mjamzito wiki ya 15 sasa ila jmn hali yake haitaki kabisa kuimarika ni kutapika nyongo japo kwa sasa sio kila siku sasa kinachonileta kwenu ni rangi husika ya nyongo akianza kutapika inakuwa njano ile kali akiendelea inakuwa ya kahawia sasa je hii ni kawaida au ni tatizo na yanatoka mengi

Lakini jambo lingine ni kiungulia jamn analalamika wakati mwingine anasema anaungua kwenye koo kuna vidonda yaani hata sielewi kwa mfano jana usiku hakula kabisa.

kaka na dada zangu nahitaji mnishauri kwa lolote na huu ni ujauzito wake wa kwanza.... niambieni nimtayarishie nini kwani damu ipo 9.5 akinywa hemovit anatapika.. mimi hadi nakosa lakufanya...... NAOMBENI MSAANA WENU JAMANI
 
wewe huu mda wa kuja kuandika mtandaoni ungekua ushafika hospitali,,,sasa subiri ushauri mpaka jioni sawa,,,,,,
 
wewe huu mda wa kuja kuandika mtandaoni ungekua ushafika hospitali,,,sasa subiri ushauri mpaka jioni sawa,,,,,,
Tumeshaenda saana na jumatatu tulikuwa huko wanasema itaisha kutapika ni kawaida na kiungulia ni kawaida ...... ndio maana nimekuja humu pia ili kupata mawazo ya madaktari wengine na wamama au wadada wenye uzoefu wa hali hii.
 
Maji ya hiliki anywe.
Asinywe maji baridi.
Matunda na mboga mboga kwa wingi.
Awe na kitu anafanya asikae tuuu akayasikiliza maradhi
Afanye mazoezi lazima asubuhi na jioni.
Aachane na vitu vyote vyenye gesi.
Kitunguu thom ni dawa sana ila kwa saivi itakuwa ngumu kwake.
 
Mpeleke kwa daktari mwingine. ..kwa opinion nyingine. .inasaidia. .wengine huwa wanamwekea drip ili asiwe dehydrated. ..MOLA awe nanyi. .upendo wako kwa dada yako ni mkubwa sana. .ubarikiwe ndugu yangu
 
Mpeleke hospitali tu, isije kuwa ni mimba ya Alliens
 
*Hiyo ya kutapika nyongo kama kazidi mkacheck na malaria.
*Mjitahidi kumwepusha na vitu au vyakula au hali zinazopelekea kichefuchefu na hata kutapika.
*Aavoid pia vitu vyenye sukari nyingi kama juice za viwandani.
*Hemovit angeacha kwa muda (mimi ilinishinda kila nknywa natapika nkaona ntapungukiwa tu maji na virutubisho vngne nikaacha na vile vidonge pia niliacha,nlipata nafuu nkakomaa na rosela na matunda,maini,nyama,supu ya maharage,mayai ila vidonge vya follic acid asiache)
*Maji yabaridi yanapunguzaga kichefuchefu kuliko kunywa maji ya kawaida.
*Uwe naye karibu kumfariji na kumtia moyo.
*Msiache kumwomba Mungu ampe wepesi ktk kipindi hiki cha baraka.
 
Well said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…