Msaada kwa mjane anayedhulumiwa

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,804
Reaction score
10,715
Wakuu, nimetakiwa kumsimamia mama mjane juu ya haki zake. Mama huyu aliolewa mwaka 1997 huko Mpanda na mume aliyekuwa na watoto wanne wakubwa. Baada ya mwaka mmoja mume aliyekuwa mfanyakazi alipewa redundance.

Wakaamua kuhamia DSM. Alitangulia mwanamume akatafuta nyumba ya kupanga. Wakati huo walikuwa na mtoto mdogo ambaye alifariki baadaye. Mume alimfuata mke wakaja kuishi DSM ambapo walizaa mtoto mmoja aliye sekondari hata sasa.

Mume alipata kazi ya korokoroni aliyokuwa akiendelea nayo hadi mauti ilipomkuta.

Wakiwa DSM walifanikiwa kujenga nyumba huko mbagala ambapo walikuwa wakiishi hadi mauti yalipomfika mume. Kazi ya mwanamke ni mganga wa tiba za asili.

Shida ni kuwa watoto wale wa mama wa kwanza pamoja na shehe (mume alikuwa mwislamu) wanadai kuwa nyumba waliyoijenga ni mali ya watoto pamoja na vitu vingine vyote. Huyu mama wanasema akabidhiwe kwa ndugu zake wao wauze nyumba watoto wagawane pesa. Wanasema huyu mama akaolewe tena huko kwao ilhali kajijengea nyumba na mumewe ili waishi hati mpaka mauti yawafike.

1. Je, sheria ya kiislamu inasemaje juu ya hili? Huyu mama aliyetumia muda na nguvu zake kujijenga na mumewe ni sahihi afukuzwe hapo?

2. Sheria za nchi zikoje katika hili? Mwanamke keshanyang'wa hati za nyumba na watoto, ingawa anao ushahidi tosha kuwa hiyo nyumba kaijenga na mumewe.

3. Leo ndio kuna kikao cha ukoo cha maamuzi, nahitaji msaada wa haraka katika hili.

MziziMkavu, @hofsfede nsajigwar Mtambuzi, Bikra figganigga VoiceOfReason gscan, Mwangaruka
 
Last edited by a moderator:
hakuna shehe anayeweza kufanya hivyo, labda kama hatumii kuran. hapo itatakiwa mirathi ya kiislam ambayo mjane kama kweli anatambulika katika ndoa ya kiislam, atakuwa na portion yake kabisa imeshaandikwa kwenye sheria za kiislam.

by the way, i am interested kuwa huyo mjane ni mganga wa jadi....hahaha. mwambie awaone mashehe/makadhi wakubwa kwa huyo anayeamua hivyo watamsaidia
 
Msaada uliopo hapo ni kuwa Huyo Mama Atafute Wakili na afunguwe kesi mahakamani ya kuwashitaki hao watoto wanaotaka kumnyang'anya hiyo nyumba ya mume wake atapata haki zake bila ya hivyo hapo ni inaonyesha anadhulumiwa huyo Mama na hao watoto.
 
Ngoja nikae kimya sio fani yangu mimi, pole sana kwa matatizo
 
msimamizi wa mirathi ya marehemu ameshateuliwa na makama?? kama bado mama apeleke maombi ya zuio la kutenda lolote juu ya mali mahakamani ikiambatana na maombi ya yeye kuteuliwa msimamizi wa mirathi au mtu mwingine anayemuamini,
kama nyumba inahati milki (kama nimekuelewa) apeleke zuio kwa msajili wa hati ili kuzuia uwezekano wowote wa kuhamisha mali.

baada ya mume kufariki, haki za mwanamke wa kiislamu (aliyeolewa) zipo wazi katika Quran.
 
Kwakweli kesi/kadhia kama hizi, Vijana haswa wakiume huwa wanakuwa na tamaa na mara nyingi kudhulumu wandugu na wazazi !!
Solution apeleke mashataka yake katika Ustawi wa jamii na Mahakama (polisi) !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…