Huyo mdada amefanya makosa makubwa sana. Kwanini amesubiri mtoto mpaka amefikia umri wa miaka mitano? Mume wake amemzoea na anajua ni mtoto wake na pia amemuhudumia kwa kila kitu. Leo ghafla aambiwe kuwa mtoto si wako hapo ni mauaji tu!!!!! Hakuna muamana hapo. Kingine hata mtoto mwenyewe naye aambiwe huyu si baba yako ila baba yako ni huyu, kwa kweli kisaikolojia mtoto ataadhirika. Katika hali ya kiubinadamu mtu utakayekuwa naye tangu mdogo kwa ukaribu hata kama si ndugu yako lakini tangu utoto mlikuwa pamoja, mkasoma wote hadi chuo, kiukweli mnakuwa na upendo mkubwa sana kuliko ukioneshwa ndugu yako ukubwani, inakuwa vigumu kuwa na upendo kama yule rafiki yako uliyekuwa naye tangu utotoni.
ushauri:
wazazi wa mke wakutane na wazazi wa mume wazungumze kwanza; nina hakika hakitaharibika kitu watalumbana, lakini hatimaye watafikia muafaka. Baada ya muafaka wa wazazi, hapo ndipo wazazi wa mume wakae waongee na mwanao wamfahamishe hali halisi ya kuwa mtoto si wake, najua atapaniki lakini lazima hatimaye atafikia muafaka na wazazi wake. Hayo yote yakifanyika hakutatokea madhara ya mauaji bali talaka inawezekana ikatokea.
Huyo mke naye aache ukware, yeye ameolewa anahangaika nini? Na wewe kijana nawe una mke ukware wa nini?