Msaada kwa mke wangu pls!

Msaada kwa mke wangu pls!

France Noel

Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
17
Reaction score
3
Salamu nyingi zikufikie hapo ulipo.

Dhumuni langu na shida yangu kuu ni kuomba msahada wa mawazo na kitaalamu. Kunatatizo limemtokea mke wangu, kwani linapelekea kunichanganya mimi na yeye pia. Kwa kifupi nikwamba;tulikuwa tunategemea kupata mtoto, nibaada ya yeye kuniambia anahisi mabadiliko flani ndani ya mwili wake ikiwapo chuchu kumuuma, na kuhisi mabadiliko ya tumbo lake kwa kuongezeka ukubwa tofauti na kawaida.

Kingine nikwamba ameshindwa kuziona siku zake kama kawaida, kwani alizoe kuziona tarehe 6 mwezi wa2 na tarehe 4mwezi wa3, kwa mwezi wa4 alitegemea labda angeziona kwanzia tarehe 2 lakini ikawa tofauti. Ndipo tukajipa matumaini uwenda wife amekwisha nihifazia ndani kiumbe changu, furaha tele zikanitoka, zawadi nyingi nikawa na mletea.Lakini leo nimeshtuka baada ya kuniambia anatokwa na damu ukeni!

Nikiangalia tarehe inasema tarehe 13/4, sasa mbona sielewi kwanini yanatoke aya tena? ndipo nikaamua kutafuta ushauri umu kabla sijafanya lolote.

Naombeni ushauri wenu wanajamvi.
 
Wewe nawe una vituko sana!

Yaani kukosa siku kwa wiki mbili tu tayari umehitimisha kwamba ana mimba? Inaonekana huna experience ya kutosha na wanawake. Huwa inatokea wakarusha hata mwezi mzima halafua ikaendelea tena. Si lazima awe amepata mimba. Kwanini uishi kwa kuhisi wakati vipimo vya mimba vimejaa kwenye kila pharmacy.

Kwanini msingepima, baada ya kuona hapati siku zake? Wala hakuna tatizo, ni jambo la kawaida tu kwa mwanamke.
 
Nami ndio nmeshangaa,vipimo sh 500 tu unampima mwenyewe afu mnaishi kwa kuhisi!?
 
Mkuu pole.Kitaalam huenda mkeo ana tatizo la Amenorrhea(Kukosa hedhi hadi kufikia miezi 3 hv).Kwa maelezo yako yawezekan
 
wewe nawe una vituko sana! Yaani kukosa siku kwa wiki mbili tu tayari umehitimisha kwamba ana mimba? Inaonekana huna experience ya kutosha na wanawake. Huwa inatokea wakarusha hata mwezi mzima halafua ikaendelea tena. Si lazima awe amepata mimba. Kwanini uishi kwa kuhisi wakati vipimo vya mimba vimejaa kwenye kila pharmacy. Kwanini msingepima, baada ya kuona hapati siku zake? Wala hakuna tatizo, ni jambo la kawaida tu kwa mwanamke.

nashukuru kwa kunifumbua juu ya kurusha siku,ila mwezi mgeni katika mambo hayo. Pia ndio mbia yake ya kwanza toka tuwe kwenye ndoa takribani miaka 4
 
...a pia alipatwa na Ectopus Pregnancy(Kutungwa nje ya mji wa uzazi/placenta).Ni pm ili niongee nawe unwkee no yako pia
 
nashukuru kwa kunifumbua juu ya kurusha siku,ila mwezi mgeni katika mambo hayo. Pia ndio mbia yake ya kwanza toka tuwe kwenye ndoa takribani miaka 4

Eeh, kweli inaonekana ni experience mpya. Lakini pia inaweza kutokea kwamba mimba imetungwa nje ya tumbo la uzazi. Lakini hii huwa ni kesi tofauti. Katika incidence kama hii, damu zinaweza kuendelea kutoka huku mimba bado imo ndani. unaweza kununua kipimo ukacheki hata kama kuna damu. Kama mtakuta ana mimba basi itabidi mmuone daktari kwa ushauri.

Depending on how it is situated, daktari anaweza kupendekeza itolewe au muendelee nayo. Lakini akisema muiache, itamaanisha kwamba mkeo awe kwenye bed rest kuanzia miezi kadhaa kabla ya kujifungua. Nadhani madaktari watasema zaidi, mimi naandika kutokana na experience tu.
 
Mtu anatokwa damu unaomba msaada humu
Nendeni hospital mkirudi ndo tushauriana
Pole itakua amepata miscourage
Salamu nyingi zikufikie hapo ulipo.Dhumuni langu na shida yangu kuu ni kuomba msahada wa mawazo na kitaalamu. Kunatatizo limemtokea mke wangu,kwani linapelekea kunichanganya mimi na yeye pia.Kwa kifupi nikwamba;tulikuwa tunategemea kupata mtoto,nibaada ya yeye kuniambia anahisi mabadiliko flani ndani ya mwili wake ikiwapo chuchu kumuuma,na kuhisi mabadiliko ya tumbo lake kwa kuongezeka ukubwa tofauti na kawaida. Kingine nikwamba ameshindwa kuziona siku zake kama kawaida,kwani alizoe kuziona tarehe 6 mwezi wa2 na tarehe 4mwezi wa3,kwa mwezi wa4 alitegemea labda angeziona kwanzia tarehe 2 lakini ikawa tofauti. Ndipo tukajipa matumaini uwenda wife amekwisha nihifazia ndani kiumbe changu,furaha tele zikanitoka,zawadi nyingi nikawa na mletea.Lakini leo nimeshtuka baada ya kuniambia anatokwa na damu ukeni!Nikiangalia tarehe inasema tarehe 13/4,sasa mbona sielewi kwanini yanatoke aya tena?ndipo nikaamu kutafuta ushauri umu kabla sijafanya lolote. Naombeni ushauri wenu wanajamvi
 
Nami ndio nmeshangaa,vipimo sh 500 tu unampima mwenyewe afu mnaishi kwa kuhisi!?
Nadhani huyu jamaa anapenda kujaza crappy things kwenye kichwa chake, sasa na hili nalo linawezaje kukusumbua kichwa wakati ni almost bure??? Hizo hela anazotumia kunnua mizawadi si angezitumia kwanza kwenye kuconfirm kitaalamu???

Hata hivyo, inawezekana kabisa mtu akawa mjamzito na bado akabreed, hii ni abnomality ila nimeshawahi experience hii kitu particularly kwa mimba changa. Kubwa ni kuwaona wataalam ili washauri ipasavyo.
 
Back
Top Bottom