Msaada kwa Mtoto anakojoa damu

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,162
Reaction score
9,073
Mtoto wangu ana mwaka mmoja na miezi mitano na ni wa kiume,mwezi mmoja uliopita alikuwa anakojoa huku kachuchumaa nje nikamuona last drop ilikuwa na wekundu wa Sami,nikamwambia wife akakataa na kutoamini!!

Wiki mbili zilizopita akashikwa na joto kali na kutapika kwa kila alichokula ndani ya dakika 10-15,akipewa maji alitapika,akinyonya pia alitapika na chakula ndio kabisaa!! Nikampeleka hospital ya gvt wakasema hana malaria labda UTI,wakampa dawa akatumia ikaisha na nikanunua tena ili kutimiza dozi!!

Baada ya siku kadhaa akaumwa tRNA,nikampeleka private hospital,wakasema ana malaria na pampasi aliyovaa aliikojolea mkojo usiku asubuhi ikawa ni chafu nikamuonyesha Dr ila akasema nisihofu mtoto mdogo hapati UTI!!

Leo asubui wife yupo safarini mkoani ananiambia bukta ya mtoto kaikuta na damu damu alipomalizs kukojoa!!!

Wakuu tatizo itakuwa ni nini??!! Naomba mnisaidie!!
 
Pole sana mkuu ni vyema ukampeleka mtoto hospitali na akaonwa na daktari atafanyiwa assessment na atafanyiwa vipimo. Nikushauri tafuta pediatrician Yaani daktari wa watoto.
 
Wahi kwa dk wa watoto. Masawe kinondoni au amil pale upanga watakusaidia sana
 
rRNA ndio nini? unamaanisha Transfer RNA!! But pole mkuu, hivi huko hospital alipimwa kweli au ndio hawa madaktari wakukisia ugonjwa. Mtoto apimwe tena mkojo na damu hapo lazima kuna tatizo.
 
Pole sana mkuu ni vyema ukampeleka mtoto hospitali na akaonwa na daktari atafanyiwa assessment na atafanyiwa vipimo. Nikushauri tafuta pediatrician Yaani daktari wa watoto.

Asante Mkuu,jana amepelekwa tena hospital pale tabata shule na kupimwa mkojo ila ikaonekana upo safi tu,yaani hana maambukizi,Dr akashauri mtoto apewe maji ya kunywa mengi na machungwa!!
 
Wahi kwa dk wa watoto. Masawe kinondoni au amil pale upanga watakusaidia sana

Asante mkuu ila makazi yangu ni Tanga,wife yupo Dar kwa ajili ya usaili wa kazi tu,ila ntaendelea kufanya jitihada!!!
 
rRNA ndio nini? unamaanisha Transfer RNA!! But pole mkuu, hivi huko hospital alipimwa kweli au ndio hawa madaktari wakukisia ugonjwa. Mtoto apimwe tena mkojo na damu hapo lazima kuna tatizo.

Mkuu RNA ilikuwa ni typing error,nilimaanisha akaumwa tena!!

Mkuu,jana amepelekwa tena hospital pale tabata shule na kupimwa mkojo ila ikaonekana upo safi tu,yaani hana maambukizi,Dr akashauri mtoto apewe maji ya kunywa mengi na machungwa!!
 
sawa mkuu pole kwa kuuguza.
 
Dx Schistosomiasis

Ddx UTI
 
Asante mkuu ila makazi yangu ni Tanga,wife yupo Dar kwa ajili ya usaili wa kazi tu,ila ntaendelea kufanya jitihada!!!
km yupo Dar mwambie amuulizie Dr Massawe anajulikana sana sio hapo Dar tu hata sisi huku Dodoma
UTI huo ugonjwa una homa kali sana na unawashika wototo wadogo na kuwamaliza nakuomba nenda kwa wataalamu zaidi na Dawa zake zipo maduka mengi, kwani umesema ni tatizo la mkojo
 
Asante kwa ushauri na mda wako mkuu!!
 
Dx Schistosomiasis

Ddx UTI

kivipi patient with UTI anakuwa na Haematuria...?? kwa schistomiasis hapi nakuunga mkono...mkojo wenye damu alwys huwa ni main indicatory na schistosoma Haematobiam( urinary Bladder trematoda) ushauri wangu kwa muhusika aende na sample ya urine ya mtoto ika fanyiwe urine examination kuona eggs of Schistosoma....au Sericariae larva......!!! Iwapo ata bainika ana schistosomiasis Dawa ni PRAZQUANTEL mg 40.
 
UTI kama differential mkuu,

Urine inatakiwa midstream urine, Praziquantel 40mg/kg 6hrly divided dose
 
Mwanangu pia alikua na hyo tatizo, kapona sasa , ntafute nkushaur 0713781217
 
UTI kama differential mkuu,

Urine inatakiwa midstream urine, Praziquantel 40mg/kg 6hrly divided dose

Mkuu mtoto wa mwaka mmoja kichocho atoe wapi, tena dar es saalam hii, alipata swimmers itch wapi?...alafu pia schistosomiasis doesnt come with that fever, unless its katayama fever ambayo haiko kwenye bladder ila kwenye liver caused by mansoni au japonicum but not heamatobium!

My take, huyo mtoto ana uti tu!...tena kwa umri huo nawasiwasi bado hajatairiwa which could be the source of infection!

Apelekwe hospital apewe gentamicine 7.5mg/kg once daily for 7 days...hio ndo dawa inauwezo wa kucover wadudu wengi!....dawa aloyopewa mwanza nahisi haikuwa broad ndio maana hakupona vizuri!
 
Peleka mtoto Hospitalini wacha udandala wa kuna kuuliza huku.....
 
Then how to r/o schistosomiasis with blood in urine?

Acute Glomerulonephritis? ( in severe cases)

Nephrotic Syndrome? ( in most cases)

But no other signs to support the above dx.

UTI???
 
Then how to r/o schistosomiasis with blood in urine?

Acute Glomerulonephritis? ( in severe cases)

Nephrotic Syndrome? ( in most cases)

But no other signs to support the above dx.

UTI???

High fever, vomiting everything na hio urinary symptom, all lead to a urinary tract infection!...

i dont see why you can think of schistosomiasis kwa age aliyonayo mtoto na mazingira pia without Ruling out UTI kwanza!

Na Kwa acute gromerulonepritis it has to be very severe for you to appriciate blood kwenye urine (na at that stage inakua imefika kwenye nephritic syndrome not nephrotic) , most of the time inakuaga ni microscopic, and in that case am sure angekua anahistoria ya kuvimba...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…