Katika hili kuwekewa' X' si utaratibu sahihi. utaratibu ni kwamba kama serikali inataka kuchukua ardhi itatoa notisi kwa wakazi wa eneo linalochukuliwa na kutoa siku ya mwisho wa kuondoka (deadline). kabla ya watu wanaostahili kulipwa kuondoka serikali inatakiwa iwe imewalipa waathirika ndani ya wiki sita. zikipita wiki sita waathirika wana haki ya kufungua kesi ya madai mahakamani dhidi ya serikali. Angalia kifungu na. 13 cha sura ya 118 shiria za Tanzania.