Ndugu wanajanvi naomba msaada kwa anaeifaham vizuri biashara ya mbao zakupaulia nyumba.
Naomba kufaham nitaifanyaje ili iweze kunilipa?
Mtaji wake ili niweze kuanza vizur nianze na Tsh ngapi?
Kwasasa nina mashine yakuranda pamoja na mashine yakupasulia mbao naamini hizi ni miongoni mwa nyenzo ambazo zinahitajika ili nipate kuanza biashara hiii.
Asanteni!
Kwanza naomba nikuulize swali, utapata wapi mbao ulizotaja? Maana kupata Lory la mbao aina hiyo ni kazi kubwa sana, kwa pale Dsm huwezi kupata kabisa, labda kama mtu alizitunza, kwa ufupi ni kwamba misitu ya mbao hizo haipo kwa sasa. Zamani ilikuwa kule west kilimanjaro. Na michache iliyooteshwa na watu ilishavunwa.
Japokuwa ipo kidogo sana, yaani mti mmoja mmoja, Ukienda Ng`ang`ange Kilolo waweza pata kidogo.
Mimi nadhani una maanisha pines, pines ndio hizo zimejaa Buguruni na kwingineko, lakini cyprus ni habari nyingine kabisa.
Asante bwana malila kwa maelezo yako yenye kutia moyo.Kwakweli umenifungua macho kwani nilimaanisha pines ila nilifikir ndizo wanazoziita cyplas.
Naomba sasa unipe uelewa wako juu ya biashara hii ya hizi mbao za pines kwani kwa maelezo ulioyatoa inaonesha unauelewa juu ya biashara hii.
Asante